MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA AKAMATWA NA POLISI....

Kamatakamata ya Viongozi wa CHADEMA baada ya vurugu huko Kahama na Iringa imeendelea hii leo baada ya mbunge wa Arusha mjini kamanda Godbless Lema kukamatwa na Polisi...

Hivi sasa anahojiwa na Jeshi la Polisi nitaendelea kuwajuza zaidi...



Mbunge wa Arusha Mjini aliyekua ameitwa kituo kikuu cha Polisi Arusha mapema leo, ameachiliwa baada ya mahojiano ya muda mrefu na. Kamanda wa upelelezi kituoni. Hapo. Pichani Lema kwenye gari lake akitoka polisi mchana huu..
Continue Reading...

Tuhuma za Zitto Kabwe kutoka kimapenzi na mbunge Catherine Magige ( CCM ) ni za uongo na zimepikwa kwa lengo la kumchafua....


KUNDI la watu ambao inadaiwa kwamba wamekula yamini ya kumchafua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa namna yoyote ile, wamemuonjesha machungu Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.

Zitto, baada ya msululu wa tuhuma ambazo nyingi zilibainika kupikwa makusudi ili kuichafua taswira yake mbele ya jamii, sasa hivi anahusishwa kutoka kimapenzi na Magige, ikidaiwa kuwa walisafiri pamoja kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya mambo yasiyofaa.
 
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti LA Uwazi umebaini kuwa tuhuma hiyo ya Zitto na Magige ni nyingine kati ya zile zilizopikwa, kwani ukweli wake ni wa kufikirika.
 
Imebainika kuwa safari ya Dubai ambayo inasemwa kuwa Zitto na Magige walisafiri, inapotoshwa kwa sababu ukweli ni kwamba wabunge hao walisafiri pamoja na timu nzima ya Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni (PAC) kwa shughuli za kikazi na hakukuwa na suala la mapenzi kati yao.

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC, akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu kama hicho.
  
 “Nimeona wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai. Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. Zitto ndiye hakwenda Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini.
 
“Katika hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui, siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea. Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.”
 
Mjumbe wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara, alisema: “Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma  pengine wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa.
 
“ Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu. Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje, huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema).
 
“Kitendo cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo, tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. Safari zote huwa analala na dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo, namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.”
  
 Zitto hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza: “Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi.”
Continue Reading...

SAD:- Mzee Dude wa FUTUHI afariki dunia

 


MSANII wa kundi maarufu la vichekesho na uigizaji la Futuhi, Mzee Dude amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza leo jioni..
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
Continue Reading...

CHADEMA kususia uchaguzi mkuu wa 2015 iwapo Serikali haitaboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura..Soma Zaidi Hapa


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa sharti ambalo kama halitatekelezwa chama hicho hakitashiriki Uchaguzi Mkuu wala hakitapiga kura ya kupitisha rasimu ya katiba. 
 
Sharti hilo lilitolewa mjini Bukoba juzi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo mikutano ya Operesheni ya M4C Pamoja Daima uliofanyika katika Uwanja wa Mashujaa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
 
Alisema chama hicho hakitashiriki uchaguzi iwapo Serikali haitaboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu na upigaji kura wa rasimu ya katiba.
 
Mbowe alisema kwa jins hali inavyoonesha Serikali haioneshi nia ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati tunaelekea katika uchaguzi Mkuu mwakani.
 
Alisema katika utafiti wao wamebaini kuwepo kwa vijana zaidi ya milioni 5.3 ambao wamefikisha umri wa miaka 18 wanaotakiwa kushiriki kupiga kura mwakani kuchagua viongozi wao.
 
Alisema katika hilo nchi itasimama kwa vile kama tunahitaji mabadiliko hayawezi kufanyika bila kuboresha daftari la kura. Kuhusu Rasimu ya Katiba, Mbowe aliapa mbele ya mkutano huo kuwa mwaka huu ndio atang’olewa meno bungeni, kwani hawatakuwa tayari kuburuzwa wakati wa Bunge la Katiba lijalo .
 
Alisema:“Suala la katiba halina masihara ni maisha yenu, maisha ya watoto wenu, maisha ya vizazi na vizazi, ni maisha ya taifa letu kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 wa kupiga kura lazima apige kura kukubali rasimu ya katiba mpya, nasi Bungeni hatutakubali kuburuzwa. ”
 
Alisema kutokana na hali hiyo, wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kujadili rasimu ya katiba mpya. Alisema bunge lijalo la katiba wao wanaenda kujadili rasimu ya Katiba Mpya ambayo tayari wameshaona .
 
“Tayari CCM wanampinga Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuhusiana na maoni ya wananchi kutaka serikali tatu, wakati wao haimo kwenye sera yao, hapa kuna tatizo, kwani sisi tunaenda kujadili maoni yawananchi wengi si kutetea sera za vyama vya siasa,” alisema.
 
Alisema katiba si suala la kidini, sera za vyama vya siasa wala la kikabila , bali ni ya watu wote kwa ajili ya mustakabali wa maisha na taifa kwa ujumla, hivyo hawaendi Dodoma kwa ajili ya kupinga Katiba hiyo, bali kupitisha maoni ya wananchi wanavyotaka.
 
Pamoja na mambo mengi, Mbowe aliwapongeza madiwani wa Manispaa hiyo bila kujali itikadi za vyama kuungana kupinga ufujaji wa kodi za wananchi maskini wa Manispaa uliokuwa ukifanyika ndani ya Manispaa hiyo.
 
“Mimi napenda kuwapongeza Madiwani wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Mbunge wao, Balozi Kagasheki, ambao kwa pamoja walisimama kutetea maslahi ya wananchi wa Bukoba, ukweli tuuseme na mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni,” alisema.
 
Wakati huo huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu, amewaonya baadhi ya wanasiasa wanaotumia makanisa na misikiti kuwashawishi wananchi ili wawachague kuwa viongozi katika uchaguzi wa mwaka huu 2014/15.
 
Lissu aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza katika mikutano miwili iliyofanyika katika Kijiji cha Ilongero na Mjini Singida juzi wakati akiwa kwenye siku ya kwanza ya ziara ya ujumbe wa chama hicho ikiwa ni mwendelezo wa Operation M4C Pamoja Daima itakayofanyika nchi nzima.
 
Alisema kuwa pamekuwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa Wakristo na Waislamu ambao hupita makanisani na misikitini na kutoa fedha kwalengo la kujijengea umaarufu jambo ambalo aliwataka wananchi wawe macho nao.
 
Alisema pamoja na wanasiasa hao kujiwekea mazingira ya kushawishi wananchi ili wawachague, Watanzania hawawakubali kwani hiyo inaweza kuleta tofauti za kidini.
 
“ Lazima tukumbuke mafundisho ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ambayo yalisisitiza kuzingatia amani, upendo na mshikamano kwa kuepuka kugawanywa na watu hao,” alisema.
 
Kuhusu Katiba Rasimu ya Pili ya Katiba, alisema ni nzuri na kuzingatia vipengele vingi vilivyotolewa maoni kurekebishwa kazi ambayo ilifanywa na CHADEMA pamoja na wananchi wengine.
 
Alisema suala kubwa ni kuona kuwa Rasimu hiyo haichakachuliwi kwa manufaa ya chama cha siasa au viongozi kwa ajili ya maslahi yao.
“Tunasisitiza kuwepo kwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kuboreshwa ili wananchi wengi wakiwemo vijana waliofikia umri huo na wale waliopoteza shahada zao waweze kushiriki katika zoezi laku pigakura za maoni,”alisema.

Katika hatua zingine , Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa, John Henje, alisema chama hakitavumilia mtu yeyote anayetaka kukizamisha chama hicho. “Mtu yeyote akileta mchezo atafukuzwa, CHADEMA itaendelea kwani hakuna aliye mkubwa au maarufu kuliko wanachama,” alisema. Alieleza kuwa chama hicho kitaendelea kuwepo na kinachotakiwa sasa ni kuzungumzia mambo ya msingi yanayokijenga na kukiendeleza.

Continue Reading...

PICHA:- Rose Ndauka amwanika binti yake "Naveen" hadharani....

 
Rose  Ndauka ambaye ni mama anayetamba ndani  ya filamu za kibongo hivi karibuni alijifungua mtoto wa kike na kumpa jina la Naveen.



Upekuzi  wa  mtandao  huu  umefanikiwa   kuinasa  picha  ya  Naveen  ikiwa  mtandaoni   kama  inavyoonekana  hapo  chini....


Siku  chache  baada  ya  kujifungua, Rose  Ndauka  aliwaonya   wasanii wa kike kuachana na biashara ya utoaji mimba kwani ni kinyume cha maadili ya  mtanzania .

Ndauka alisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu nyota hawataki kuzaa, hata wale waliozaa kabla ya kuwa nyota hawapendi kujulikana kama  wamezaa, kitu ambacho hakinamaana  yoyote  katika maisha ya msanii
Continue Reading...

Tanzania Kuisaidia Madagascar Kuondolewa Vikwazo Ilivyowekewa Na Jumuiya Za Kimataifa... Soma Zaidi Hapa

 
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013.
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo.
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa Madagascar waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini. Picha na 5 na 6. Viongozi mbalimbali na wanachi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina mjini Antananarivo.

Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Madagascar katika masuala mbalimbali  na kuhakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo na jumuiya za kimataifa vinaondolewa kufuatia nchi hiyo kurejesha utawala wa kidemokrasia.



Akizungumza katika mahojiano maalum  mjini Antananarivo, Madagascar, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amesema kuwa sasa serikali ya Madagascar imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano sio tu na Tanzania bali nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya za kimataifa.



Waziri Membe ambaye alikuwa amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Madagascar Bw. Hery Rajaonarimampianina zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo jana  amesema kuwa Tanzania imefurahishwa na hatua hiyo na kuongeza kuwa huo ni ushindi mkubwa kwa SADC.



Amesema kuwa mwaka 2009 Madagascar iliingia katika machafuko yaliyosababisha serikali halali iliyokuwepo madarakani ya Rais Mark Ravalomanana kupinduliwa na kufafanua kuwa Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Kitengo cha Amani na Usalama cha nchi za jumuiya ya SADC (TROIKA) imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inapatikana nchini humo.



“Kiongozi mpya wa Madagascar aliyepatikana na kuapishwa ni ushindi kwa Tanzania kwa sababu Rais Jakaya Kikwete amejihusisha sana na upatikanaji wa kiongozi huyo, kama tunakumbuka rais Kikwete alimuita nchini Tanzania kwa mazungumzo rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajoelina mara nne, mazungumzo haya yamezaa matunda tunayoyaona leo” amesema Mh. Membe.



Amefafanua kuwa yapo mambo makubwa ambayo Tanzania imeyafanya kufanikisha kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Madagascar ikiwemo upatikanaji wa katiba  ambayo ilikamilika mwezi wa 8 mwaka 2013 ,kufanikiwa kuwashawishi Andry Rajoelina na Mark Ravalomanana waliokuwa mahasimu kutoshiriki kugombea katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.



Amesema Tanzania imefurahishwa na kitendo cha rais Andry Rajoelina aliyeingia madarakani kwa kufanya mapinduzi kukubali kuachia madaraka na kuachia utawala wa demokrasia utawale nchini humo.



Ameeleza kuwa Tanzania sasa iko tayari kushirikiana na Madagascar na kama mjumbe wa SADC itahakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo vinaondolewa pia kuhakikisha kuwa kiongozi huyo mpya anashiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika utakaoanza tarehe 30 mwezi huu.



 “Tulimwahidi rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajolina kuwa atakapotekeleza hayo tunayoyataka ikiwemo kuanzisha mchakato wa katiba,  kuruhusu utawala wa demokrasia, na kuruhusu uchaguzi ili kupata rais mpya sisi tutakuwa mstari wa mbele kushawishi nchi za SADC na nchi za AU kuwaruhusu kushiriki mikutano yote ili waweze kuijenga nchi yao na jambo hilo tutalifanya ” amesisitiza Mh.Membe.



Katika houtuba yake mara baada ya kuapishwa rais Rajaonarimampianina amesema kuwa utawala wake unaanza ukurasa mpya wa kuijenga upya nchi hiyo iliyokuwa imegawanyika kisiasa na kusababisha chumi wake kudorora huku akiueleza umati mkubwa wa watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake kuwa ataongeza mapambano dhidi ya rushwa na kuleta amani, utulivu na maridhiano kwa mustakabali wa taifa hilo.



Madagascar ambayo sasa inaingia katika utawala mpya wa rais Hery Rajaonarimampianina ambaye hapo awali alikuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo iliingia katika machafuko yaliyosababisha kuondolewa kwa utawala wa rais Mark Ravalomanana aliyekimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini.



 Hery Rajaonarimampianina  akiungwa mkono na rais aliyepita Andry Rajoulina anakuwa rais wa 4 wa nchi hiyo  kufuatia ushindi  mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013 uliompatia  asilimia 53.3  dhidi ya mpinzani wake Bw. Jean Louis Robinson aliyepata asilimia 46.5
Continue Reading...

"CHADEMA haina uwezo wa kushika Dola Kutokana na Mfumo wake wa utawala kuwa mbovu unaotokana na udikteta, udini na ukabila ".... Asema Elizabeth Minde



Chama  cha  mapinduzi  ( CCM)  manispaa  ya  Moshi  mkoani  Kilimanjaro   kimeendelea  kusisitiza  kuwa  chama  cha  demokrasia  na  maendeleo, CHADEMA   hakitaweza  kushika  dola  kutokana  na  mfumo  wake  wa  utawala  kuwa  mbovu....

Kauli  hiyo  ilitolewa  jana  na  mwenyekiti  wa  CCM manispaa  ya  Moshi, Elizabeth Minde  wakati  alipokuwa  akimnada  mgombea  wa  udiwani  wa  kata  ya  Kiboriloni  kwa  tiketi  ya  chama  hicho, Willy Adriano...

Mwenyekiti  huyo  alisema  migogoro  inayoendelea  ndani  ya  chama  hicho  ni  ishara  ya  utawala  mbovu  unaotokana  na  udikteta, udini  na  ukabila, hivyo  chama  hicho  kupewa  dola  ni  kuhatarisha  amani  ya  nchi  hii  ambayo  imekuwa  nembo  ya  taifa  hili  kimataifa...

Alisema  CCM imejipanga  vya  kutosha  kupata  ushindi  katika  uchaguzi  huo  huku  akiwatahadharisha  wanaoibeza  CCM  kuwa  tayari  kuingia  aibu  ufikapo  februari 9  maka  huu...

"Ili  mwananchi  aweze  kupata  maendeleo  tunahitaji  kupata  kiongozi  makini  ambaye  ataweza  kuwaletea  wananchi  maendeleo, hivyo  nawaomba  wananchi  wa  kata  ya  Kiboriloni  wamchague  Willy Adriano, CCM ushindi  unakuja"..Alisema  Minde

Kwa  upande  wake  katibu  mwenezi  wa  CCM mkoa, Michael  Mwita, alisema  kazi  ya  CCM ni  kuisimamia  serikali  katika  kutekeleza  shughuli  za  kimaendeleo  kutokana  na  ilani  ya  chama  hicho.

"Asilimia  90  ya  wakazi  wa  Kiboriloni  wanakabiliwa  na  changamoto  lukuki, huwezi  kuwa  na  mbunge  ambaye  ana  maslahi  yakwake.Kuna  wapanda  mlima  wamekuwa  wakinyanyasika  na  malipo  yao  duni, lakini  imekuwa  ngumu  kwa  mbunge  huyo  kuwatetea  vijana  hao" Alisema  Mwita

Aliongeza  kuwa  mbunge  huyo  tangu  achaguliwe  mwaka  2000  hakuna  maendeleo  yoyote  aliyowaletea  wananchi  wa  Moshi  pamoja  na  kutoa  ahadi  lukuki  ikiwemo  ahadi  ya  kurudisha  soko  la  Kiboriloni  ambalo  kwa  sasa  limehamishwa.

Alisema  mbunge  huyo  hana  nia  ya  dhati  ya  kuwakomboa  wananchi  wake  tofauti  na  anavyodai  katika  majukwaa  ya  siasa  na  kuongeza  kuwa  mwaka  2010  aliwaahidi  wamachinga  kuwa  endapo  watamchagua  na  kumpa  halmashauri  atahakikisha  machinga  hawanyanyaswi  huku  akiahidi  kuwajengea  machinga  complex, ahadi  ambayo  haijatekelezwa  hadi  sasa.

Continue Reading...

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro Kwa Mara Ya Kwanza Aitembelea tume ya mabadiliko ya katiba....



Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) akipokea nakala za ripoti za Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiwemo Rasimu ya Katiba kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Tume hiyo aliyoifanya mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Saalam.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) wakati alipowasili katika Ofisi za Tume hiyo kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Ofisi hiyo katika ziara yake aliyoifanya mwishoni mwa wiki. (PICHA NA TUME YA KATIBA)
Continue Reading...

Tuhuma nzito Baraza la Mawaziri , Profesa Ibrahim Lipumba Atilia shaka elimu ya waziri wa fedha..



MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.

Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.

Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.
 

Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.

“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.

Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.

“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.

Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.

Alisema kutokana na hali hiyo, uamuzi wa Serikali wa kuwaondoa mawaziri mizigo hautafanikiwa kwa sababu waziri huyo anaweza kuongeza mzigo mwingine kwa nchi.

“Mawaziri mizigo, wanaisababishia Serikali kuwa na viongozi mizigo, hivyo basi tunapaswa kuwa makini kwa kupinga kuongozwa na viongozi mizigo, kwa sababu wanaweza kutuletea matatizo,” alibainisha.

Akitolea mfano katika kipindi ambacho Waziri wa Fedha anapaswa kuwa makini na matumizi ya fedha za Serikali, ni pamoja na kuwepo kwa mchakato wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura, mchakato wa Bunge maalumu la Katiba, vitambulisho vya uraia na mambo mengine ambayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji fedha.

Alisema kutokana na hali hiyo, waziri huyo anapaswa kusimamia matumizi ya fedha katika shughuli mbalimbali zikiwemo za halmashauri na safari za Rais, ambapo katika kipindi hiki cha robo mwaka, safari zake za nje zimemaliza bajeti yake ya mwaka mzima.

Alisema kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete alipaswa kumchagua mtu makini mwenye sifa stahiki kukalia nafasi hiyo, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa kufuata taratibu za kisheria.

Alisema chama hicho hakina mashaka na uteuzi wake, lakini wana mashaka na chuo alichosoma na kupata shahada ya kwanza na ya pili.
 
WAZIRI AJIBU
Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.

Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.

“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.

“Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya.

>>Mtanzania
Continue Reading...

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, Akiri kwamba Serikali ilifanya uzembe katika kutatua taarifa za uchochezi zilizosababisha vurugu za Mtwara.., Soma Zaidi



WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amekiri kwamba Serikali ilifanya uzembe katika kutatua taarifa za uchochezi zilizosababisha vurugu za Mtwara. Kauli hiyo aliitoa mjini Mtwara  jana alipozungumza na wananchi wa Masasi akiwa njiani kuelekea wilayani Nanyumbu kufungua mradi wa umeme. Alisema baada ya kutokea kwa uzembe huo wako wajanja wachache waliotumia nafasi hiyo kufanikisha malengo yao.

“Katika hili tulizidiwa ujanja na watu wengine kwa kuwa walikuwa wakiwaambia wananchi kwamba gesi itatolewa Mtwara na kupelekwa Dar es Salaam.

“Tena wakasema ikishafikishwa Dar es Salaam ambako vitajengwa vinu na gesi nyingine itapelekwa Bagamoyo kwao Rais Jakaya Kikwete.

“Huo ulikuwa ni upotoshaji mkubwa tena mkubwa kweli lakini sisi tulilichukulia juu juu, hatukutazama kwa undani kulieleza hilo na wajanja wakalipata na kulipotosha hilo,” alisema Pinda.

Alisema gesi itazalishwa Mtwara ingawa vinu vitajengwa Dar es Salaam kwa ajili ya kuisambaza gesi hiyo kwa watumiaji wengine.

“Wakati nazungumza na watu wa Mtwara mwaka jana, walinieleza mambo mengi sana juu ya hiyo gesi na mwishowe nikawauliza hivi kwanini hamtaki gesi itoke Mtwara.

“Nikawauliza, hivi ikija meli hapa Mtwara ikapaki pale bandarini na kupakia gesi na kuipeleka Uarabuni mtakataa, wakasema hatuna shida, nikawauliza tena je, meli hiyo hiyo ikipakia gesi na kuipeleka Dar es Salaam, mna tatizo, wakasema hatuna tatizo.

“Sasa nikawauliza tatizo lenu ni nini, wakasema ni hilo bomba lenu hilo mnalojenga. Mimi nikawaambia gesi itazalishwa hapa Mtwara, tena katika Kijiji cha Madimba na itakayopelekwa Dar es Salaam haitazidi asilimia 10.

“Nikawambia gesi ikianza kuzalishwa mtanufaika kwa kuwa hata viwanda vitakuwapo kikiwamo cha Dangote kitakachozalisha saruji pale Kijiji cha Msijute,” alisema Pinda.

Kuhusu hasara iliyopatikana baada ya wananchi kufanya vurugu na kuharibu mali, alisema bado inafanyiwa kazi na itakapokamilika italetwa mkoani Mtwara.

“Baada ya vurugu zile, Serikali ilifanya tathimini ya matukio na ikiwezekana kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha huu itakuwa imekamilika na tutaangalia la kufanya ingawa nataka niwahakikishie kwamba jambo hili tunalifanyia kazi na litakapokamilika tutalirudisha kwenu,” alisema Pinda.

Aliwashukuru viongozi wa Mkoa wa Mtwara kwa kutochukua uamuzi wa kulipa kisasi wakati wa vurugu hizo kwa kuwa kama wangeamua kufanya hivyo hali ingekuwa mbaya zaidi.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Farida Mgomi, alisema vurugu hizo zilizotokea Januari 26, 2013 zilisababisha hasara ya Sh bil 3.4.

>>Mtanzania
Continue Reading...

Chadema waitaka CCM isikwamishe Katiba Mpya

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) naSerikali yake kuacha kile alichokielezea kuwa ni hila ya kutaka kukwamisha mchakato wa Katiba Mpya.
Mchakato huo sasa unaelekea katika hatua ya Bunge Maalumu la Katiba. Amesema Watanzania hawako tayari kurudi nyuma kuendelea na katiba ya sasa.
Alikuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara huko Ngara, mkoani Kagera juzi, ambao ni sehemu ya operesheni ya Movement For Change (M4C) iliyopewa jina la ‘Pamoja Daima’.
Mbowe alisema yupo tayari kuwa wa kwanza kufungwa kwa kosa la kudai Katiba Mpya kama Serikali itaweka mazingira ya hila ambayo yatalazimisha kukwamisha mchakato wa kupata Katiba Mpya na kuwafanya Watanzania kuendelea na Katiba ya mwaka 1977.
Alisema watawala wasitumie hila na mwanya wowote kuitia nchi majaribuni kwa kulazimisha watu kuishi na katiba iliyokosa uhalali wa kisiasa na kisheria.
Alisema badala yake, wanatakiwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira mazuri kwa Watanzania kujiamulia nama ya kuongozwa
Kiongozi huyo wa Chadema alisisitiza kuwa Katiba ni uhai wa taifa na si matakwa ya chama chochote cha siasa wala mtu binafsi.
Alisema Watanzania wengi wamependekeza kuwapo kwa shirikisho la Serikali tatu katika Rasimu ya Katiba Mpya, lakini akadai kuwa zipo njama zinazofanywa za kuchakachua uamuzi huo wa wananchi kwa ajili ya kukilinda CCM. Alisema kama hila hizo za kupindua maoni ya wananchi zitafanikiwa kupenyezwa kupitia bungeni, yuko tayari kuungana na Mtanzania yeyote kuzunguka nchi nzima kuwahamasisha wananchi waikatae rasimu hiyo.
Alisisitiza kwamba endapo wananchi wataikataa Katiba hiyo, pia hawatakuwa tayari kurudi kuendelea kutumia katiba ya zamani inayotumika hivi sasa kama ambavyo Serikali imekwishasema.
“Watawala lazima wajue. Watanzania hawa ambao wameipigania na kuililia Katiba Mpya kwa muda mrefu sasa hawako tayari tena kurudi nyuma,” alisema kiongozi huyo wa Chadema
-mwananchi

Continue Reading...

Utekaji malori wasababisha maelfu kukwama Nzega

Zaidi ya magari 1,000 yamekwama kwenye Barabara Kuu ya Mwanza - Dar es Salaam katika Kijiji cha Ngonho, Kata ya Miguwa, wilayani Nzega, kutokana utekaji wa malori uliofanywa juzi usiku.

Baadhi ya madereva walisema walikutwa na mkasa huo juzi saa nne usiku wakati magari yao yalipotekwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi na kuwanyang’anya mali na kisha kuwatendea ukatili wa kuwajeruhi sehemu mbalimbali za miili yao ikiwa ni pamoja na kuwakata masikio na kuwatoboa macho.

Kutokana na tukio hilo, waligoma kuondoa magari yao na kusababisha mabasi ya abiria na malori ya mizigo kukwama wakati abiria wapatao 3,000 wakitaabika kwa kukosa chakula na maji.

Madereva hao waligoma kuondoa magari yao baada ya kukasirishwa na kitendo cha polisi wa Nzega kushindwa kuwasaidia wakati walipotekwa.

Madereva hao wameapa kutoondoa magari hayo hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe au Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa watakapofika kwenye eneo hilo ili kusikiliza kilio chao.

Unyama wa watekaji

Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, Emmanuel Mihayo alisema watu walijeruhiwa vibaya kwenye utekaji huo kwa kukatwa masikio na kutobolewa macho.

Dk Mihayo aliwataja majeruhi hao kuwa ni raia wa Burundi, Herelina Eddy, ambaye alitobolewa macho na hali yake ilikuwa mbaya na alikuwa kwenye maandalizi ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga kwa matibabu zaidi.

Alisema majeruhi wengine wawili wanaendelea vizuri na matibabu katika hospitali hiyo. Majeruhi hao ni Abraham Ismail na Omary Adrian, ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Alisema Adrian alikatwa sikio na shavu pamoja na mkono wa kushoto wakati Ismail alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.

Polisi watuhumiwa

Mmoja wa madereva waliotekwa, ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa alisema kuwa polisi wa Nzega waliombwa kutoa msaada lakini walikataa.

Dereva huyo alisimulia kuwa mmoja wa madereva alifanikiwa kutoroka wakati walipotekwa na kwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nzega lakini askari waliokuwepo kituoni hawakutoa ushirikino.

“Polisi hao walitoa visingizio, wakidai kwamba gari lao halina mafuta na walikataa kutumia lori la dereva huyo kwenda kwenye eneo la tukio,” alisimulia dereva.

Baada ya kunyimwa msaada, dereva huyo alilazimika kurudi kwa wenzake ndio akajikuta akitekwa tena.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Peter Ouma, ambaye alifika kwenye eneo la tukio, aliahidi angewachukulia hatua kali polisi hao.

“Nawaahidi ndugu zangu, hawa waliosababisha hali hii wote nawachukulia hatua kali za kinidhamu mara mmoja na taarifa hizi mtazisikia kwenye vyombo vya habari,” aliahidi Kamanda Ouma, huku akiwaomba madereva wa malori na magari ya abiria waendelee na safari zao.

Hata hivyo, madereva hao waligoma kuendelea na safari na badala yake walisisitiza kuwa wanataka askari waliokuwa doria wachukuliwe hatua za kinidhamu.

“Tunalishangaa Jeshi la Polisi, wameshindwa kutusaidia na matukio kama haya yamezidi hapa Nzega tunataka Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani wachukue hatua... hatuondoki mpaka kieleweke,’’ alisema dereva mwingine, ambaye pia aligoma kutaja jina lake.

Madereva hao walisema vitendo vya utekaji magari katika Wilaya ya Nzega, vimekuwa vikitokea mara kwa mara na kuhatarisha maisha ya watu, magari na mali zao.

“Hivi mbona tukiendesha magari haya na kwenda nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hatupati matatizo haya ya kutekwa,” alihoji dereva mwingine.

Mateso kwa abiria

Kutwa nzima jana, mabasi na magari madogo yalikwama katika eneo hilo na kusababisha foleni kubwa, hivyo kusababisha adha kwa wasafiri, hasa wanawake na watoto.

Kutokana na hali hiyo, wachuuzi wa bidhaa mbalimbali walitumia fursa hiyo kujineemesha kwa kuuza vitu kwa bei ya juu, ambapo chupa ya maji ya kunywa nusu lita iliuzwa Sh1,000 badala ya Sh500 wakati ile ya lita moja Sh2,000 badala ya Sh1,000.

Aina zote za soda ziliuzwa Sh2,000 badala ya kati ya Sh600 hadi 1,000 wakati sahani moja ya chakula kwa mamalishe iliuzwa kati ya Sh3,000 na Sh5,000.

Mmoja wa abiria alionekana akilalamika na kutoa maneno makali ya kuwashutumu madereva kwa kuwasababisha adha hiyo pamoja na Serikali kushindwa kuwasaidia.

“Sisi tunataabika, hatuna msaada. Watoto wetu wanateseka, wengi wetu tumeishiwa, hatuna fedha,” alilalamika Mariamu Majara, abiria aliyekuwa akisafiria kwenye basi la Kajumulo lililotoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.

Continue Reading...

Bunge la Katiba Kizungumkuti,

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba bado ina upungufu ambao utaathiri utendaji wa Bunge Maalumu, ambalo huenda likaanza Februari 11 mwaka huu, mjini Dodoma.

Sheria hiyo Namba 8 ya 2011, imeishafanyiwa marekebisho mara mbili yakiwamo ya Februari 2012 na Novemba 2013, lakini mabadiliko hayo yameacha kasoro ambazo zinapaswa zifanyiwe tena kazi, kupitia Bunge.

Kasoro zipo katika Kifungu cha 22 kinachohusu uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum, pamoja na kifungu cha 24 kinachozungumzia Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo wanavyoanza kutekeleza wajibu wao.

Kupitia Sheria ya Marekebisho (Na:2) ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2013, Bunge katika mkutano wa 12, liliwapa mamlaka Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, ‘kufanya maandalizi muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Bunge Maalumu’.

Watendaji hao kwa mujibu wa sheria ndio watakaoteuliwa kuwa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalumu baada ya Rais kutangaza kuitishwa kwa Bunge hilo, lakini kiapo chao kitasubiri hadi pale watakapochaguliwa Mwenyekiti na Makamu wa Bunge hilo.

Sheria husika inaweka sharti kwamba ikiwa Mwenyekiti atatoka upande mmoja wa Muungano basi Katibu atoke upande mwingine na kinyume chake. Hivyo lazima wasubiri uchaguzi huo ili wajue ni nani Katibu na Naibu Katibu.

Kifungu cha 24 (2) kinasema: “Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalumu, watashika nyadhifa zao kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atachaguliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano basi Katibu wa Bunge Maalumu atatoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano”.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa tayari baadhi ya wataalamu kutoka Ofisi ya Bunge na ile ya Baraza la Wawakilishi (BLW) wameanza maandalizi ya awali katika moja ya hoteli za jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah mbali na kukiri kuanza kwa maandalizi hayo, hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani suala hilo kwa maelezo kuwa lazima ashirikiane na Katibu wa Baraza la Wawakilishi. 

Hata hivyo, kutokana na mkanganyiko mkubwa uliopo katika Sheria hiyo, ni dhahiri watendaji hao watapata wakati mgumu katika kuanza kutekeleza majukumu, hasa katika kuteua wajumbe wa sekretarieti ya Bunge hilo.

Uteuzi wa wajumbe hao kwa mujibu wa kifungu cha 24 (4) unapaswa kufanywa na  Katibu kwa kushauriana na Naibu wake, nafasi ambazo hazitakuwapo hadi pale Mwenyekiti na Makamu wake watakapochaguliwa.

Fursa ya marekebisho

 

Hivi sasa hakuna fursa kwa Bunge la Muungano kufanya marekesho katika sheria hiyo ili kuondoa mkanganyiko uliopo, kwani kikao chake ambacho kilipaswa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu hadi mwanzoni mwa Februari, kilifanyika Desemba mwaka jana, ili kutoa fursa kwa  Bunge Maalumu.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alisema jana kuwa ikiwa kuna kasoro zozote zitakazojitokeza, wataalamu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wale wa Baraza la Wawakilishi watazifanyia kazi.

“Kuwapo kwa upungufu katika sheria zinazotungwa huwa ni jambo la kawaida, lakini pili katika sheria huwezi kuandika kila kitu na ndiyo maana katika mabadiliko yaliyofanyika Katibu wa Bunge na mwenzake wa Baraza la Wawakilishi walipewa wajibu wa kisheria kufanya maandalizi,” alisema Kairuki na kuongeza:

“Na tulifanya hivyo makusudi kwani tunata uzoefu uliopo katika vyombo hivi utumike katika kuendesha Bunge la Katiba, mimi ninawaamini wataalamu wetu kwa hiyo hakuna kitakachoharibika.”

Vifungu vinavyokanganya

Kifungu cha 22 kimeweka masharti kwamba baada ya kuitishwa kwa Bunge hilo, Katibu wa Bunge la Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, watasimamia mchakato wa kumchagua Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalumu.

Kadhalika, kifungu cha 24 (5) cha Sheria hiyo kinasema: “ Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum, kabla ya kushika madaraka yao wataapa au kula yamini mbele ya Rais”. Kwa maana hiyo, watendaji hao watasimamia uchaguzi wa mwenyekiti wa muda pasipokuwa  na nguvu ya kisheria kwani watakuwa hawajala kiapo kutokana na kutofahamu nafasi zao; ni yupi Katibu na Naibu Katibu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa muda ambaye anachaguliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (a) na (b), ndiye atakayesimamia uandaaji na upitishwaji wa Kanuni za Bunge Maalum na kuendesha uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Lakini ni dhahiri kwamba Mwenyekiti wa muda atachaguliwa bila kuwapo kwa kanuni, huku kukiwa hakuna utaratibu wowote wa kisheria anaoelekeza jinsi atakavyopatikana.

Kadhalika kifungu cha 26 (1) cha Sheria hiyo kinataka shughuli zote za Bunge Maalum ziendeshwe kwa kufuata Kanuni husika na pia kifungu cha 24 (3) kinawataka watendaji watatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Kanuni hivyo uchaguzi wa Mwenyekiti wa muda na usimamizi wake lazima vizingatie kanuni jambo ambalo haliwezekani kwani zitakuwa hazijapitishwa.

 

Continue Reading...

KIGOGO WA WEMA NOMA SANA.. AFANIKIWA KUMNASA RAFIKI WA WEMA ....

Tatoo ya Clement Mgongoni Mwa Naima
Stori: Imelda Mtema
NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).

“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement  kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.

NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.

“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.

“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.

“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.

WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.

“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.

UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.

Alipoulizwa kuhusu  tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).

“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.

WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.

Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.

“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.

NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.

“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.
“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu.
Continue Reading...

ASKARI MAGEREZA MBARONI KWA KUUA MFUNGWA ...

Msemaji wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omary Mtiga
Askari Magereza wanane, wamefikishwa mahakamani wilayani Mafia mkoani Pwani kwa tuhuma za mauaji ya mfungwa.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi wa Wilaya ya Mafia, Hassan Makube, ilidaiwa kuwa, Desemba 19 mwaka jana, askari hao walimuua Basiri Makungu aliyekuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Kilombero, lililopo kwenye wilaya hiyo. Askari waliofikishwa mahakamani hapo walitajwa kuwa ni Sajenti Sadick na wenzake ambao walifunguliwa kesi namba 1/2014.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja walimuua Makungu, baada ya kumshambulia kwa kipigo mwishoni mwa mwaka jana.

Kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu, pamoja na kesi ya mauaji kutokuwa na dhamana, watuhumiwa hao walirudishwa rumande hadi Februari 7 mwaka huu.

Akizungumzia tukio hilo, ofisa wa juu wa Jeshi la Magereza, Menrad Tesha alisema kuwa, jeshi hilo linafahamu taarifa za askari hao kushtakiwa kwa makosa hayo, lakini akasema suala hilo halipo chini yao. Tesha alipohojiwa kuhusu mustakabali wa ajira za askari hao na iwapo wanashtakiwa kama raia au wafungwa alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa sasa.

“Siwezi kuzungumzia ajira zao hapa, huu siyo utendaji unaotakiwa, kila kitu kina taratibu zake, hivyo siwezi kulizungumzia hilo,” alisema Tesha.

Alieleza kuwa askari anapotuhumiwa kwa makosa yoyote suala lake huachwa mikononi mwa vyombo vinavyostahili, ili kuwachukulia hatua.

“Hivi sasa wale ni watuhumiwa, kwa hiyo mimi kuliongelea siyo sahihi. Kama kuna kitu ungetaka kufahamu, basi nakushauri mfuate mkuu wa gereza kule walipo sasa (Mafia), atakueleza kila unachotaka kufahamu kuhusu askari hao kwani bado wapo huko,” alisema Tesha.

Matukio ya Askari Magereza kuua wafungwa

Februari mwaka jana ilidaiwa kuwa Willfred Mallya mwenye namba 315 aliyefungwa mwaka 2003 katika katika Gereza la Kisongo mjini Arusha aliuawa kutokana na kipigo cha Askari Magereza.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Omary Mtiga licha ya kukiri kutokea kwa kifo cha mfungwa huyo, alikanusha kuwa kilitokana na kipigo cha askari hao akisema kifo chake kilikuwa ni cha kawaida.

Desemba mwaka 2010, askari wanne wa jeshi hilo waliokuwa wakifanya kazi katika Gereza la Lilungu mkoani Mtwara, walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji ya mfungwa.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Abdulhaman Mohamed mbele ya Hakimu Stepheni Mbungu.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Oktoba 31, mwaka 2010 watuhumiwa hao kwa pamoja walimuua mfungwa aliyekuwa na namba 215, Kasimu Kumchaya
Continue Reading...

PENNY:AFUNGUKA NA KUSEMA DIAMOND KAMA CHIZICHIZI VILE...., ILA ....


MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel Ten, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa sifa ya aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni kama chizichizi lakini kwa undani zaidi ni mtu makini.

Penny alifunguka hayo mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo mbali na kutamka kauli hiyo, alifunguka mambo mengi yaliyohusu penzi lao ambalo alilitaja kuwa wamelipumzisha kwa kupeana nafasi.
Akizungumzia sifa za staa huyo aliyeogelea naye penzini kwa kipindi cha mwaka mmoja na ushee hivi, Penny alisema watu wote wanamjua Diamond ni kama chizichizi vile kutokana na mapepe anayoyafanya akiwa mzigoni lakini linapokuja suala la uhusiano, anakuwa makini sana.
“Diamond ni kama chizichizi vile lakini kwa ndani ni mtu makini sana. Anajua kulea, anajua umuhimu wa mapenzi na anaelewa anatakiwa kumfanyia nini mpenzi wake anapokuwa nyumbani, anajali,” alisema Penny na kuongeza:

“Watu wamuanavyo nje na jinsi alivyo katika maisha ya kawaida ni tofauti kabisa, mapepe anayafanya anapokuwa jukwaani na sehemu nyingine zinazohusu kazi yake na si nyumbani.”
Katika aya nyingine, Penny alitiririka na mistari kuwa, baada ya kuona penzi lao limetawaliwa na misukosuko, walikaa chini kwa pamoja na kuamua kupeana nafasi ya kila mmoja wao kufanya mambo yake, hakuna kati yao aliyemtamkia mwenzake kuwa sikutaki.
Alisema katika maisha huwa hapendi vitu vya kuambiwa, hata aliposikia taarifa za Diamond kurudiana na Wema kwa mara ya kwanza nchini China, hakuamini hadi walipokuja kukaa naye na kuzungumza ndipo walipoamua kupeana nafasi.


Hata hivyo, Penny alisema anaamini kuwa Diamond amerudiana na Wema lakini yeye kwa sasa ‘bado yupoyupo sana’, akakiri kuwa anatongozwa na watu tofauti na endapo ikitokea akaamua kuanzisha uhusiano mpya, hatahitaji mtu maarufu kwani anahitaji maisha yake kuwa ya siri, tofauti na zamani. 
GPL
Continue Reading...

Ufoo Saro wa ITV amwaga machozi kanisani wakati akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumnusuru alipopigwa Risasi na mchumba wake... SOMA ZAIDI HAPA

Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba Jimbo la Magharibi Ufoo huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema "Ni miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo"
 
Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili hospital aliwashukuru watu wote waliomtia moyo na kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa.

Ufoo saro jana  amefanya ibada na kusema "Namshukuru Mungu kwa kuniponya"... Hiii ni mara ya kwanza kwa Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.

 "Sina cha kuwalipa,ninawashukuru sana kwa wema wenu pia kwa kuniombea .Mungu ni mkubwa na amenipigania naendelea vizuri kwa sasa .Mungu alinisimamia na nyinyi pia mliniombea hakika sina budi kushukuru kwa kila jambo,nitasoma zaburi ya 146 katika Biblia Takatifu ili kumshukuru Mungu kwa kunisaidia".
 
Ufoo alisema kuwa ameamua kumshukuru Mungu kwa sababu siyo watu wote wanaopata matatizo kama yake na wakapona.
 
Mchungaji wa kanisa hilo Joseph Maseghe aliyeongoza misa hiyo iliyofanyika jana  asubuhi  alisema Mungu hakupanga Ufoo afariki dunia kwa kupigwa risasi. "Mungu bado anakuhitaji, hakupanga ndiyo maana upo nasi leo hautakiwi kulia huu ni mwanzo wa maisha yako mengine usilie unachotakiwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo".alisema  mchungaji huyo.
 
Misa hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyakazi wa ITV pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Grace Kihwelu akiwemo na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) John Heche.Baada ya kukamilika kwa misa hiyo ndugu na marafiki wa karibu wa Ufoo walijumuika pamoja kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana.

Continue Reading...