CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa sharti ambalo kama halitatekelezwa chama hicho hakitashiriki Uchaguzi Mkuu wala hakitapiga kura ya kupitisha rasimu ya katiba.
Sharti
hilo lilitolewa mjini Bukoba juzi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
Mbowe, wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo
mikutano ya Operesheni ya M4C Pamoja Daima uliofanyika katika Uwanja wa
Mashujaa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Alisema
chama hicho hakitashiriki uchaguzi iwapo Serikali haitaboresha Daftari
la Kudumu la Wapigakura wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu na upigaji
kura wa rasimu ya katiba.
Mbowe
alisema kwa jins hali inavyoonesha Serikali haioneshi nia ya kuboresha
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati tunaelekea katika uchaguzi Mkuu
mwakani.
Alisema
katika utafiti wao wamebaini kuwepo kwa vijana zaidi ya milioni 5.3
ambao wamefikisha umri wa miaka 18 wanaotakiwa kushiriki kupiga kura
mwakani kuchagua viongozi wao.
Alisema
katika hilo nchi itasimama kwa vile kama tunahitaji mabadiliko hayawezi
kufanyika bila kuboresha daftari la kura. Kuhusu Rasimu ya Katiba,
Mbowe aliapa mbele ya mkutano huo kuwa mwaka huu ndio atang’olewa meno
bungeni, kwani hawatakuwa tayari kuburuzwa wakati wa Bunge la Katiba
lijalo .
Alisema:“Suala
la katiba halina masihara ni maisha yenu, maisha ya watoto wenu, maisha
ya vizazi na vizazi, ni maisha ya taifa letu kila Mtanzania mwenye umri
wa miaka 18 wa kupiga kura lazima apige kura kukubali rasimu ya katiba
mpya, nasi Bungeni hatutakubali kuburuzwa. ”
Alisema
kutokana na hali hiyo, wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kujadili
rasimu ya katiba mpya. Alisema bunge lijalo la katiba wao wanaenda
kujadili rasimu ya Katiba Mpya ambayo tayari wameshaona .
“Tayari
CCM wanampinga Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba kuhusiana na maoni ya wananchi kutaka serikali tatu, wakati wao
haimo kwenye sera yao, hapa kuna tatizo, kwani sisi tunaenda kujadili
maoni yawananchi wengi si kutetea sera za vyama vya siasa,” alisema.
Alisema
katiba si suala la kidini, sera za vyama vya siasa wala la kikabila ,
bali ni ya watu wote kwa ajili ya mustakabali wa maisha na taifa kwa
ujumla, hivyo hawaendi Dodoma kwa ajili ya kupinga Katiba hiyo, bali
kupitisha maoni ya wananchi wanavyotaka.
Pamoja
na mambo mengi, Mbowe aliwapongeza madiwani wa Manispaa hiyo bila
kujali itikadi za vyama kuungana kupinga ufujaji wa kodi za wananchi
maskini wa Manispaa uliokuwa ukifanyika ndani ya Manispaa hiyo.
“Mimi
napenda kuwapongeza Madiwani wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Mbunge
wao, Balozi Kagasheki, ambao kwa pamoja walisimama kutetea maslahi ya
wananchi wa Bukoba, ukweli tuuseme na mnyonge mnyongeni na haki yake
mpeni,” alisema.
Wakati
huo huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA),Tundu Lissu, amewaonya baadhi ya wanasiasa wanaotumia makanisa
na misikiti kuwashawishi wananchi ili wawachague kuwa viongozi katika
uchaguzi wa mwaka huu 2014/15.
Lissu
aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza katika mikutano miwili
iliyofanyika katika Kijiji cha Ilongero na Mjini Singida juzi wakati
akiwa kwenye siku ya kwanza ya ziara ya ujumbe wa chama hicho ikiwa ni
mwendelezo wa Operation M4C Pamoja Daima itakayofanyika nchi nzima.
Alisema
kuwa pamekuwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa Wakristo na Waislamu
ambao hupita makanisani na misikitini na kutoa fedha kwalengo la
kujijengea umaarufu jambo ambalo aliwataka wananchi wawe macho nao.
Alisema
pamoja na wanasiasa hao kujiwekea mazingira ya kushawishi wananchi ili
wawachague, Watanzania hawawakubali kwani hiyo inaweza kuleta tofauti za
kidini.
“
Lazima tukumbuke mafundisho ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius
Nyerere ambayo yalisisitiza kuzingatia amani, upendo na mshikamano kwa
kuepuka kugawanywa na watu hao,” alisema.
Kuhusu
Katiba Rasimu ya Pili ya Katiba, alisema ni nzuri na kuzingatia
vipengele vingi vilivyotolewa maoni kurekebishwa kazi ambayo ilifanywa
na CHADEMA pamoja na wananchi wengine.
Alisema
suala kubwa ni kuona kuwa Rasimu hiyo haichakachuliwi kwa manufaa ya
chama cha siasa au viongozi kwa ajili ya maslahi yao.
“Tunasisitiza
kuwepo kwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kuboreshwa
ili wananchi wengi wakiwemo vijana waliofikia umri huo na wale
waliopoteza shahada zao waweze kushiriki katika zoezi laku pigakura za
maoni,”alisema.
Katika
hatua zingine , Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa, John
Henje, alisema chama hakitavumilia mtu yeyote anayetaka kukizamisha
chama hicho. “Mtu yeyote akileta mchezo atafukuzwa, CHADEMA itaendelea
kwani hakuna aliye mkubwa au maarufu kuliko wanachama,” alisema.
Alieleza kuwa chama hicho kitaendelea kuwepo na kinachotakiwa sasa ni
kuzungumzia mambo ya msingi yanayokijenga na kukiendeleza.
0 comments:
Post a Comment