Chama cha mapinduzi ( CCM) manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kimeendelea kusisitiza kuwa chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA hakitaweza kushika dola kutokana na mfumo wake wa utawala kuwa mbovu....
Kauli
hiyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,
Elizabeth Minde wakati alipokuwa akimnada mgombea wa udiwani wa
kata ya Kiboriloni kwa tiketi ya chama hicho, Willy Adriano...
Mwenyekiti
huyo alisema migogoro inayoendelea ndani ya chama hicho ni
ishara ya utawala mbovu unaotokana na udikteta, udini na
ukabila, hivyo chama hicho kupewa dola ni kuhatarisha amani ya
nchi hii ambayo imekuwa nembo ya taifa hili kimataifa...
Alisema
CCM imejipanga vya kutosha kupata ushindi katika uchaguzi huo
huku akiwatahadharisha wanaoibeza CCM kuwa tayari kuingia aibu
ufikapo februari 9 maka huu...
"Ili mwananchi aweze kupata maendeleo tunahitaji kupata kiongozi makini ambaye ataweza kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo nawaomba wananchi wa kata ya Kiboriloni wamchague Willy Adriano, CCM ushindi unakuja"..Alisema Minde
Kwa
upande wake katibu mwenezi wa CCM mkoa, Michael Mwita, alisema
kazi ya CCM ni kuisimamia serikali katika kutekeleza shughuli
za kimaendeleo kutokana na ilani ya chama hicho.
"Asilimia
90 ya wakazi wa Kiboriloni wanakabiliwa na changamoto lukuki,
huwezi kuwa na mbunge ambaye ana maslahi yakwake.Kuna wapanda
mlima wamekuwa wakinyanyasika na malipo yao duni, lakini imekuwa
ngumu kwa mbunge huyo kuwatetea vijana hao" Alisema Mwita
Aliongeza
kuwa mbunge huyo tangu achaguliwe mwaka 2000 hakuna maendeleo
yoyote aliyowaletea wananchi wa Moshi pamoja na kutoa ahadi
lukuki ikiwemo ahadi ya kurudisha soko la Kiboriloni ambalo
kwa sasa limehamishwa.
Alisema
mbunge huyo hana nia ya dhati ya kuwakomboa wananchi wake
tofauti na anavyodai katika majukwaa ya siasa na kuongeza kuwa
mwaka 2010 aliwaahidi wamachinga kuwa endapo watamchagua na
kumpa halmashauri atahakikisha machinga hawanyanyaswi huku
akiahidi kuwajengea machinga complex, ahadi ambayo haijatekelezwa
hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment