MREMBO aliyetajwa kwa jina moja la Ema aliyedai kuwa ni mchumba wa
jamaa aliyemtaja kwa jina la Amri au Mdudu amefumaniwa laivu akisaliti
penzi na mwanaume mwingine.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye Makaburi ya Buguruni, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwekewa mtego.
TAARIFA KWA OFM
Wakati makachero wa Oparesheni
Fichua Maovu wakiwa kwenye ‘patroo’ walipokea taarifa kutoka kwa chanzo
chake ambacho kiliomba wafike katika makaburi hayo ambapo kulikuwa na
fumanizi.
OFM: Fumanizi la aina gani? Isije ikawa ni wanandoa tukaingia chaka.
Chanzo: Hawa bado ni wachumba tu. Jamaa alikuwa anamfuatilia
mchumba’ke amemnasa na jamaa kwenye gari wakifanya mapenzi sasa kuna
timbwili zito.
OFM: Una uhakika na unachokisema?
Chanzo: Kama hamtaki acheni (akakata simu).
OFM KAZINI
Kwa kuwa OFM haipuuzii habari, ilimteua ‘kamanda’ wake mmoja ambaye aliwasha bodaboda na kuwahi eneo la tukio.
Huku
sekeseke likiendelea makaburini hapo, Mdudu ambaye alikuwa na jazba ya
kuibiwa ‘mali’ zake alisema kuwa alitonywa na rafiki zake kwamba
mchumba’ke huyo yupo katika Baa ya Kimboka, Buguruni akijirusha na jamaa
huyo.
Mdudu alisema aliamua kwenda katika baa hiyo na kubana sehemu huku akishuhudia kila kitu.
“Unajua nimekuwa nikiambiwa tu kuwa Ema ananisaliti lakini nilikuwa napuuzia.
“Sasa nimeamini baada ya kumshuhudia mwenyewe akisaliti penzi letu,” alisema Mdudu.
VIKAO VYA HARUSI
Alisema kuwa Ema ni mchumba’ke na anaishi na wazazi wake Buguruni-Malapa, Dar na ameshamtolea mahari.
“Ndiyo tumeanza kupanga vikao vya harusi vifanyike katika Baa ya Wazee iliyopo Ilala-Amana (Dar),” alisema.
Alisema
baada ya kuwasubiri hadi usiku wa manane, aliwaona wakiinuka na kuingia
kwenye teksi ndipo na washikaji zake nao wakachukua bodaboda na
kuifuata ile teksi kwa nyuma bila wahusika kushtuka.
WAKUTWA LAIVU
Alisema walishangaa kuona gari lile
likipaki maeneo ya Makaburi ya Buguruni kisha dereva akatoka na kwenda
kusimama mbali kidogo akivuta sigara.
“Machale yakanicheza nikawatonya wanangu kuwa tusubiri kama dakika kumi halafu tukaivamie teksi.
“Baadaye uzalendo ulinishinda ikabidi nikavamie. Ndipo tukawakuta laivu wanavua nguo wakiwa kimahaba,” alisema Mdudu.
Alisema
roho ilimuuma alipomkuta mchumba’ke huyo ambaye anampenda kwa dhati
akiwa katika hali ile, nusura apoteze fahamu na mara baada ya kuwavamia
waliwatoa nje ndipo sekeseke likaanza.
KUMBE NI MSANII!
Wakati mtiti ukiendelea, yule
mwanaume mwingine aligundulika kuwa kumbe ni msanii wa Bongo Fleva
aliyejitambulisha kwa jina la Spince Seseme.
Akihojiwa kulikoni kufumaniwa na mke wa mtu,
Spince alisema hakufahamu kama Ema ni mchumba wa mtu kwani kama
angefahamu asingetoka naye kimapenzi.
Jamaa huyo aliyeimba
Wimbo wa Ayaya akimshirikisha Ali Kiba alidai alifahamiana na Ema siku
nyingi na hawakuwahi kuvunja amri ya sita.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanaomjua jamaa huyo, eti
amekuwa akitumia umaarufu wake kupindua uhusiano wa watu na kuapa
kumkomesha.
“Kama polisi wakishindwa tutamwendea kwa babu ili ajue cha mtu mali,” alisikika brazameni mmoja.
Hata hivyo, tukio hilo lilimalizika kwa
kila mmoja kukimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni akidai kupigwa
ambapo hadi OFM inaondoka walikuwa wakichukuliwa maelezo.