Ufoo Saro wa ITV amwaga machozi kanisani wakati akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumnusuru alipopigwa Risasi na mchumba wake... SOMA ZAIDI HAPA

Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba Jimbo la Magharibi Ufoo huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema "Ni miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo"
 
Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili hospital aliwashukuru watu wote waliomtia moyo na kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa.

Ufoo saro jana  amefanya ibada na kusema "Namshukuru Mungu kwa kuniponya"... Hiii ni mara ya kwanza kwa Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.

 "Sina cha kuwalipa,ninawashukuru sana kwa wema wenu pia kwa kuniombea .Mungu ni mkubwa na amenipigania naendelea vizuri kwa sasa .Mungu alinisimamia na nyinyi pia mliniombea hakika sina budi kushukuru kwa kila jambo,nitasoma zaburi ya 146 katika Biblia Takatifu ili kumshukuru Mungu kwa kunisaidia".
 
Ufoo alisema kuwa ameamua kumshukuru Mungu kwa sababu siyo watu wote wanaopata matatizo kama yake na wakapona.
 
Mchungaji wa kanisa hilo Joseph Maseghe aliyeongoza misa hiyo iliyofanyika jana  asubuhi  alisema Mungu hakupanga Ufoo afariki dunia kwa kupigwa risasi. "Mungu bado anakuhitaji, hakupanga ndiyo maana upo nasi leo hautakiwi kulia huu ni mwanzo wa maisha yako mengine usilie unachotakiwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo".alisema  mchungaji huyo.
 
Misa hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyakazi wa ITV pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Grace Kihwelu akiwemo na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) John Heche.Baada ya kukamilika kwa misa hiyo ndugu na marafiki wa karibu wa Ufoo walijumuika pamoja kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana.

0 comments: