Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema
mchakato wa kuwapata wajumbe wa Tume ya Kimahakama ya Kuchunguza Madhara
ya Operesheni Tokomeza Ujangili umeshaanza na majina hayo yatawekwa
wazi hivi karibuni.
Jaji Werema alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa
uteuzi wa wajumbe wa tume hiyo unahitaji umakini mkubwa na majina hayo
lazima yakubaliwe na Rais, kabla ya kutangazwa.
Baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vinasema kuwa,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ana uwezo wa kuteua ofisa wa polisi kuwemo
kwenye tume hiyo, kushauriana na Rais kuhusu wajumbe hao na wajumbe wa
tume hiyo kwa sababu wanatoka katika Jeshi la Polisi wanaweza.
Kadhalika sheria hiyo inaelekeza kila mjumbe wa tume kula kiapo mbele ya Rais kabla ya kuanza kazi.
Ripoti ya Bunge
Baada ya ripoti hiyo kusomwa bungeni Desemba mwaka
jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James
Lembeli, Rais Jakaya Kikwete aliamuru iundwe tume ya kimahakama ili
kuchunguza ukweli wa ripoti hiyo pamoja na waliotajwa kuhujumu
operesheni hiyo.
Kabla ya kuhamishwa wizara, aliyekuwa Waziri wa
Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alisema mchakato wa kuundwa kwa tume
hiyo ya kimahakama huenda ukakamilika mwezi huu.
Chikawe alisema, Tume hiyo itaundwa na jaji kutoka Mahakama Kuu, wapelelezi na baadhi ya wanasheria.
“Itahusisha watu ambao watafanya kazi kisheria
zaidi kwa kuangalia kwa kina kipi kilitokea wakati wa operesheni hiyo,
ili tuufahamu ukweli kwa sababu ripoti ile kwa kweli ilitushitua,”
alisema Chikawe.
Alisema tume hiyo itapita katika maeneo yote
ambayo yametajwa kwenye ripoti na kufanya uchunguzi wa kina kubaini
iwapo kweli matukio kama hayo yalifanywa na polisi.
“Pia tume itajaribu kuangalia kama ni kweli wapo
watu ambao walikuwa wanapata yale mateso yaliyotajwa kwenye ripoti kwa
mfano mtu kulazimishwa kuchora chatu kwa kutumia kiwembe kwenye paja,”
alisema.
Chikawe alisema kama tume hiyo itagundua kuwa ni kweli polisi walifanya unyama huo basi kwa hakika hatua kali zitachukuliwa.
Alisema Tume ya Kimahakama itachunguza kwa kina madhara
yaliyotokana na operesheni hiyo iliyosababisha utesaji wa kinyama, vifo,
uharibifu wa mali na upotevu wa mifugo. Tume itachunguza waliohusika,
ikiwa ni pamoja na waliotajwa katika ripoti hiyo ya Kamati ya Bunge kwa
kuhujumu operesheni hiyo.
Matumizi mabaya ya silaha (Mfano; mzee wa miaka 70
kuuawa kwa kupigwa risasi tatu, nyumba za wananchi kuchomwa moto,
mifugo kuuawa kikatili kwa kuchomwa moto na kupigwa risasi.
Mengine ni kulazimishwa kufanya mapenzi na mti,
kufanya mapenzi na baba mkwe, na baadhi kulazimishwa kuchora chatu
kwenye paja kwa kutumia wembe.
0 comments:
Post a Comment