Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo
cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila aka VJ Penny, amesema kuwa yeye
na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana
nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.
Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum
na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo
pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema
Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia
historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na
Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za
Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.
Akizungumzia kuhusu alivyojisikia baada
ya kuona picha za Diamond akiwa na Wema, Penny amesema yeye pia
alishangaa kama watu wengine walivyoshangaa kuziona.
“Mimi ni mtu ambaye utaniambia ‘fulani
amefariki’ na sitakiamini mpaka nione kabisa huyu hapa amekufa,” amesema
Penny. “Nilipoziona picha nilishtuka kidogo, kibinadamu nilikuwa ‘Ohh
Mungu wangu kipi kinaendelea’. Lakini sijui.. Mungu wa ajabu sana,
niliichukulia kwa uzito mdogo kadri nilivyoweza, ilipita tu kama
‘shaaa’.. na dakika inayofuata (Diamond) anasema ‘ohh ni movie’. Mimi
nilikuwa kama nyie, amini usiamini ‘Ni movie okay vizuri, baby anafanya
movie’. Kwa kawaida nilitakuwa kuipokea tofauti lakini ni kama
nilishikwa na ganzi kwa muda, sikutaka kujiumiza. Kuna ‘buttom’ ambayo
nikiruhusu iniumize nitaumia, nikiamua kitu kinipite na siwezi hata
kujisumbua. Alirejea, maisha yakaendelea, nimekaa nasubiri movie hiyo.”
Penny amesema pamoja na yote hayo, maisha yaliendelea kama kawaida kati yao kama vile hakuna kilichotokea.
“Alirejea kutoka kwenye safari yake ya
movie na tuliendelea kuwa pamoja kwasababu mimi nilikuwa nani kuhukumu
tofauti? Hicho ndicho kitu nawaambia watu, sikuwepo hivyo kama anasema
alikuwa anafanya movie nitamuamini kwasababu sikuwepo. Napenda kuona
vitu mwenyewe, mimi ni mtu wa hivyo, nahukumu vitu pindi nionapo
mwenyewe. Maisha yaliendelea, tuliendelea kuwa sisi. Nilikuwa na vitu
vilivyokuwa vikizunguka kwenye mawazo yangu nje na ndani.. ‘hivi ndivyo
natakiwa kuwa?’ Watu wanadhani nina moyo wa jiwe, nina moyo, nina akili,
saa zingine inabidi nikae nifikirie, nini hiki, nini kile. Mambo
yalikuwa sawa lakini tofauti kidogo kuzingatia ukweli kwamba sikujua
nini cha kufikiria, sikujua nini cha kufanya na nilitakiwa kuchukua muda
wangu kuhakikisha kuwa sifanyi kosa lolote. Na nilikuwa bado pembeni
yake, bado nikimsupport chochote alichokuwa akikifanya iwe movie, nyimbo
zake mpya au chochote, niliendelea kuwepo kwaajili yake kuwa girlfriend
wake, rafiki yake wa dhati, mkono wake wa kulia.”
Hata hivyo Penny amesema ilifika wakati
ambapo waliona bora ‘kupumzisha’ uhusiano wao kutokana na hali halisi ya
mabadiliko yaliyokuwa yamejitokeza.
“Kama uhusiano wowote ulivyo, kuna
mwanzo na mwisho na watu wanaachana kwa sababu nyingi. Nilihisi kwamba
nahitaji kumpa nafasi, wote ni vijana na wakati mwingine tunahitaji
nafasi kugundua vitu vipya, kuona kipi hasa unachokihitaji kwenye
maisha. Unajua ukimruhusu ndege afanye vitu mbalimbali then atajua kama
‘mti huu ndio unanifaa, mti huu haunifai. Hivyo nilihisi kwamba wote
tulihitaji hicho, tulihitaji ‘space’ hivyo nikampa nafasi na mimi
nakuchukua nafasi. Huwa nawaambia watu kuwa vyovyote ilivyo, yeyote
atakayekuwa naye, nipo pembeni yake nikimshangilia kwasababu ni kweli
(Diamond) ni mtu mzuri ndani. Achana na watu wanavyomuona chizi chizi,
sahau msanii unayemjua, ana roho nzuri na anajua anachokitaka. Ni ngumu
kuacha iende.. kama ni rahisi kuacha iende basi hujampenda huyo mtu.”
Amesema kila anapoulizwa maswali ya ni
nani kati yake na Diamond aliyemwacha mwenzake, hujibu hajui kwakuwa
wamepeana tu nafasi ya kila mtu kufanya mambo yake na kuongeza kuwa bado
wanaendelea kuwasiliana huku akiwa na furaha na chochote (Diamond)
anachofanya.
Penny amesema japo ameendelea na maisha
yake lakini bado anachukua muda kufikiria nini anachohitaji maishani na
hadi sasa hajafikiria kuwa na mwanaume mwingine. “Bado, sio kwamba
sitongozwi, wanaume wanakuja lakini najaribu … hakuna mwanaume
mkamilifu, najaribu kutafuta mwanaume anayeweza kuwa mkamilifu kidogo
najua yupo sehemu.”
Ameongeza kuwa anatamani kurejea katika
maisha ya kawaida na kuwa na uhusiano na mwanaume asiye maarufu kwakuwa
kuwa na uhusiano na mtu mwenye jina kulimfanya achunguzwe muda wote na
kujikuta akikosa maisha ‘faragha’.
“Napenda kurejea kwenye maisha niliyokuwa nayo ‘it was much fun’, napenda maisha yangu ya faragha.”
Penny amesisitiza kuwa mwaka 2014 ameupanga kuwa mwaka wa kufanya kazi zaidi na anaamini utakuwa wa ushindi kwake.
“Nilijiambia mwenyewe siku ya January 1
kuwa ‘mwaka huu ni mwaka wa ushindi kwangu’ na naenda kushinda, vyovyote
vile naenda kushinda, naenda kuweka nguvu yangu yote, kwahiyo kuna
mengi yanakuja, mengi.”
0 comments:
Post a Comment