Kareny Masasy, HabariLeo, Shinyanga
— MWANAMKE mkazi wa Kata ya Lubaga, Sophia Haji (22) Manispaa ya
Shinyanga anadaiwa kupigwa na mumewe na kusababishiwa majeraha makubwa
kwa kile kilichodaiwa alichelewa kupokea simu ya mumewe.
Polisi
inamsaka mwanamume huyo, Daniel Daud ambaye kutokana na kipigo, mkewe
alitokwa na damu nyingi sehemu za siri. Kamanda wa Polisi, Mkoa wa
Shinyanga, Evarist Mangala alisema wanamtafuta mtuhumiwa afikishwe
kwenye vyombo vya sheria.
Kwa upande wake, mwanamke huyo aliyelazwa Hospitali ya Mkoa Shinyanga, aliwaambia waandishi wa habari kwamba alipigwa kutokana na kuchelewa kupokea simu ya mumewe wakati akivuka ng’ambo ya barabara.
“Nilipofika nyumbani mume wangu alianza kunipiga,” alisema. Alisema alijitetea kwa mumewe, lakini hawakuelewana, na zaidi alimtuhumu kuwa ana uhusiano na mwanamume mwingine. Kwa mujibu wa Sophia, mumewe alimfungia ndani siku mbili huku akiwa na majeraha pamoja na kumnyima chakula.
Mimi
nilichelewa kupokea simu ya mume wangu kwa sababu nilikuwa navuka
barabara ili kujiepusha na ajali, nilikuwa na wifi yangu mdogo, lakini
nilivyofika nyumbani mume wangu akawa mkali wala hakunielewa na kuanza
kunipiga,” alisema.
Alisema wifi yake alimtetea, lakini mumewe aliendeleza kipigo. Alisema baada ya kipigo hicho kuzidi, wifi yake alipiga kelele na majirani walifika kuamua ugomvi huo.
Alisema ilipofika usiku, alihisi maumivu makali mwilini akamweleza mumewe ambaye hakumsikiliza, zaidi ya kumfungia ndani siku mbili. Anna Gilbert ambaye ni rafiki wa mwanamke huyo, alisema baada ya kukaa siku mbili bila kumwona, siku ya tatu aliamua kwenda nyumbani kwake na hakumkuta mumewe.

Alisema
alisikia sauti ya mtu anayelia ndani na alipochungulia, alimuona yuko
mahututi na alichukua jukumu la kumpeleka hospitali. Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Dk Fredrick Mlekwa alikiri kumpokea
mgojwa huyo.
Alisema alimfanyia matibabu katika vidonda vyake, ambavyo vilikuwa vinatoa usaha na alikuwa na majeraha sehemu za mapajani.
Alisema alimfanyia matibabu katika vidonda vyake, ambavyo vilikuwa vinatoa usaha na alikuwa na majeraha sehemu za mapajani.
chanzo; wavuti