Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema hautahusika na malipo ya matibabu
kwa wanachama wao watakaoathirika na utumiaji wa dawa za kuongeza
maumbile.(HD)
Akizungumza
kwenye kongamano la wadau wa mfuko huo mkoani hapa hivi karibuni, Kaimu
Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini alisema mfuko
hautatoa huduma kwa mwanachama aliyeathirika na dawa za kuongeza
maumbile ambazo zimepigwa marufuku na Serikali.
Dk
Fikirini alisema mfuko huo unatoa huduma ya matibabu kwa wanachama wake,
ila hauhusiki na waathirika wa dawa zilizopigwa marufuku na Serikali
ikiwamo za kuongeza maumbile maarufu kama dawa za Kichina.
"Leo tupo
hapa pamoja ili kuzungumza nanyi wanachama wetu, kujadili na kuona
jinsi tunavyoweza kuuboresha mfuko, ila napenda kusema NHIF hautamtibu
mwathirika wa dawa za kuongeza maumbile," alisema Dk Fikirini.
Aliwataka
wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na madiwani, kuwashawishi
wajawazito kujiunga na mradi wa kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati
wa kujifungua (KFW), ambao umekuwa mkombozi kwa baadhi ya maeneo. Dk
Fikirini alisema mradi huo umekuwa ukiwanufaisha wajawazito kujifungua
salama baada ya kupata ushauri na matibabu wakati wa kliniki, hivyo
wanawake wengi hawana taarifa na mradi huo.
Awali,
Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga, Ali Makababu alisema wananchi wengi hawana
mwamko wa kujiunga, hivyo kutaka elimu itolewe shuleni, vyuoni na
kupitia matangazo ya televisheni.
Alisema hatua hiyo imesababisha kuongezeka kwa makali ya maisha.