Muigizaji wa filamu za kibongo maarufu kwa jina Jackline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya
Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao
mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao
kwa mashabiki wake.
“Mambo mashabiki zangu.sikua na njia
nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam
amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so
imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa
ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata
ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.
Kitu Muhimu
nikuwajuza nakuwaelewesha mashabiki wangu staki maswali nawapenda wote…”
Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada
huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha
abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi
karibuni.
Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?