HIVI NDIVYO RAISI WETU ALIVYOKUWA AKIONGEA NA WALEMAVU JANA ALIPOKUWA KATIKA UZINDUZI WA MKOA MPYA WA GEITA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mlemavu Debile James kutoka katika kijiji cha Bulega wilayani Bukombe Mkoani Geita muda mfupi baada ya kufungua shule ya msingi Ng’anzo iliyojengwa na kampuni ya madini ya Nsagali yenye makao yake wilayani humo.Rais Kikwete aliahidi kumpatia Bajaji Mlemavu huyo ili aweze kumudu shughuli zake za kujitafutia kipato. Rais Kikwete yupo katika ziara ya siku tano mkoa mpya wa Geita kukagua na kuzindua shughuli za maendeleo.
Wazee wa Mkoa wa Geita wakimvisha Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete vazi la kijadi wakati wa uzinduzi wa Mkoa Mpya wa Geita Jumamosi mchana
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria kuzindua Mkoa mpya wa Geita jana  mchana.Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia elimu Kassim Majaliwa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula.