FUNDI magari mkazi wa kijiweni katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bw Abdul Husein (31) amejikuta akitupwa jela mwaka mmoja na faini ya shilingi 200,000 baada kutiwa hatiani na mahakama ya mwanzo bomani kwa kosa la kutaka penzi la nguvu kwa mwanafunzi wa darasa la tano .
Fundi huyo ambaye anadaiwa kukaribishwa katika nyumba hiyo kama mlinzi wa watoto wawili akiwemo mwanafunzi huyo wa miaka 11 alitenda kosa hilo tarehe 4 mwezi huu majira ya saa 3 usiku baada ya kurejea kutoka katika shughuli zake.
Akisoma hukumu hiyo jana hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo bomani mheshimiwa Alois Masua alisema kuwa katika ushahidi ambao ulitolewa mahakamani hapo na mtoto wa kiume wa miaka 9 ulidai kuwa kijana huyo siku ya tukio baada ya kufika nyumbani alimtaka binti huyo kumpa sahani ili aweke chips ambazo alikuja nazo .
Kuwa baada ya binti huyo kumpa sahani ndani ya dakika chache aliomba kupewa maji na binti huyo alifanya hivyo baada ya kupewa maji kijana huyo alimtaka binti huyo kusogea kukaa katika kochi ambalo fundi huyo amekuwa akilitumia kama kitanda chake sebuleni kama mlizi . Binti huyo aligoma kuingia majaribuni .
Hata hivyo haikuishia hapo baada ya muda fundi huyo fataki alimtaka binti huyo kumsindikiza chooni bado binti alionyesha msimamo wa kutamani masomo yake na kugoma kumsindikiza kwa madai kuwa yeye ni binti na huyo ni mwanaume iweje aombe kusindikizwa .
Kutokana na mbinu zote kugonga mwamba ndipo fundi fataki huyo alipoamua kutumia njia ya mkato ya kumkamata kwa nguvu binti huyo na kutaka kumbaka chooni kabla ya binti huyo kuamua kupambana na kuishia kuchaniwa sketi yake .
Hali hiyo ilimfanya binti huyo kutimua mbio na kuomba msaada kwa mama yake aliyekuwa amelala chumba cha pili kabla ya mama mzazi na majirani kuamka na kumwadabisha fundi fataki kwa kumpeleka polisi.Fundi huyo ambaye anadaiwa kukaribishwa katika nyumba hiyo kama mlinzi wa watoto wawili akiwemo mwanafunzi huyo wa miaka 11 alitenda kosa hilo tarehe 4 mwezi huu majira ya saa 3 usiku baada ya kurejea kutoka katika shughuli zake.
Akisoma hukumu hiyo jana hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo bomani mheshimiwa Alois Masua alisema kuwa katika ushahidi ambao ulitolewa mahakamani hapo na mtoto wa kiume wa miaka 9 ulidai kuwa kijana huyo siku ya tukio baada ya kufika nyumbani alimtaka binti huyo kumpa sahani ili aweke chips ambazo alikuja nazo .
Kuwa baada ya binti huyo kumpa sahani ndani ya dakika chache aliomba kupewa maji na binti huyo alifanya hivyo baada ya kupewa maji kijana huyo alimtaka binti huyo kusogea kukaa katika kochi ambalo fundi huyo amekuwa akilitumia kama kitanda chake sebuleni kama mlizi . Binti huyo aligoma kuingia majaribuni .
Hata hivyo haikuishia hapo baada ya muda fundi huyo fataki alimtaka binti huyo kumsindikiza chooni bado binti alionyesha msimamo wa kutamani masomo yake na kugoma kumsindikiza kwa madai kuwa yeye ni binti na huyo ni mwanaume iweje aombe kusindikizwa .
Kutokana na mbinu zote kugonga mwamba ndipo fundi fataki huyo alipoamua kutumia njia ya mkato ya kumkamata kwa nguvu binti huyo na kutaka kumbaka chooni kabla ya binti huyo kuamua kupambana na kuishia kuchaniwa sketi yake .
Hakimu Masua alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa, fundi huyo alipotakiwa kujitetea alikana kujitetea kwa madai kuwa hawezi kuzungumza chochote katika mahakama hiyo.
Hivyo alisema kutokana na mtuhumiwa huyo kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza mahakama hiyo ilipaswa kumfunga jela kwa miaka mitano kutokana na kosa hilo la shambulio la aibu kifungu cha 135 kanuni ya adhabu namba 6 marejeo mwaka 2002.
“ Mahakama hii inakuona na hatia na hivyo inakupunguzia adhabu kutoka miaka mitano uliyopaswa kutumikia na kufungwa mwaka mmoja jela na ukitoka utatakiwa kumlipa mlalamikaji kiasi cha Tsh 200,000”