**
Shule moja ya sekondari ya wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, imelalamikiwa na wanafunzi pamoja na wazazi kuwa mabinti wanajihusisha na vitendo vya ngono vya jinsia moja (usagaji).
Akizungumza na NIPASHE mmoja wa wazazi (jina linahifadhiwa) alisema
shule hiyo imepoteza sifa kwa kuwa kuna wimbi kubwa la wanafunzi
wanaojihusisha na vitendo hivyo vya usagaji.
Alisema mtoto wake alikuwa ameanza kidato cha kwanza mwaka jana na
baada ya kumuandikisha ndipo baadhi ya watu walipomueleza kuwa shule
hiyo kwa sasa ina sifa mbaya ya mchezo ‘huo mchafu.’
"Baada ya kuelezwa nikasema nitalifanyia kazi jambo hilo hivi karibuni
katika kupekua madaftari ya mwanangu nakutana na kibarua cha mapenzi
alichoandikiwa na msichana mwenzake niliumia sana na nilitumia nguvu
kumbana bila hivyo asingeniambia," alisema
Alisema ilimbidi amhamishe binti yake na kujiunga na shule moja ya
sekondari iliyopo mkoani Tanga kwa ajili ya kuendelea na masomo ya
kidato cha pili mwaka huu.
Mzazi huyo alisema anashangazwa ni kwa nini hatua hazichukuliwi wakati
suala hilo ni la hatari kwani watoto wao wataharibika kiakili pamoja na
kimwili na wanaweza kuambukizana VVU na Ukimwi..
Alisema wakati mwanaye akisoma katika shule hiyo alikuwa akihudhuria
vikao vya wazazi mara kwa mara na kwamba kila kikao walikuwa wakifukuzwa
wanafunzi kutokana na mwenendo huo.
"Hili tatizo ni kubwa na kufukuzwa kwa mwanafunzi sidhani kuwa wanatatua
tatizo nadhani hakuna usimamizi mzuri kwani wangeweza kudhibiti kwa
haraka tatizo hilo kabla ya kuwa kubwa," alisema
Pia alisema ndugu yake imembidi amhamishe mwanae na kumtafutia shule
nyingine kwa kuhofia binti yake kurubuniwa kwani wanakuwa ni wadogo na
hawaelewi chochote, hivyo inaweza kuwa rahisi kudanganywa na kuingia
kwenye vitendo hivyo viovu.
Alisema kuwa hata kiwango cha ufaulu kwa sasa shule hiyo imeshuka kutokana na tatizo hilo kwa wanafunzi .
Hata hivyo, NIPASHE ilizungumza na mwanafunzi mmoja ambaye anasoma
katika shule hiyo kuhusiana na suala hilo ambapo alikiri kuwepo kwa
jambo hilo na kueleza kuwa wanaofanya mchezo huo ni wa kidato cha tano
na cha sita.
"Mimi hawajanifanyia ila najua wanaofanya mchezo huo ni wale walioko
kidato cha tano na cha sita," alisema Pia kuna baadhi ya wazazi wengine
wamekuwa wakilalamikia jambo hilo na kueleza kuwa ndugu zao imewalazimu
kuwahamisha watoto wao kutokana na vitendo hivyo vinavyofanyika shuleni
hapo.
0 comments:
Post a Comment