SAFARI ya Rais Jakaya Kikwete nchini Oman imezaa matunda baada ya ujumbe wa wafanyabiashara wa nchi hiyo kutua nchini jana.
Lengo la ujumbe huo uliowakilishwa na watu 19 wakiwemo waziri
mwenye dhamana wa nchi hiyo ni kuzindua Baraza la Ushirikiano wa Oman,
Tanzania kwa masuala ya biashara ( JBC).
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa baraza hilo,
Evarist Maembe, alisema JBC inazinduliwa kwa lengo la kuimarisha sekta
ya wafanyabiashara wa nchi ya Oman na Tanzania.
Alisema uzinduzi huo utafanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo
ujumbre huo pia utapata fursa ya kukutana na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed
Gharib Bilal, pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah
Kigoda.
Maembe alisema JBC pia itaangalia namna ya nchi hizo mbili
zitakavyoshirikiana katika masuala ya huduma za kibenki, usafirishaji wa
anga, wa majini, kilimo, bima na utaalamu mbalimbali.
“Tutakachofanya sasa baada ya baraza hili ni kuhakikisha benki
zinazokuwepo nchini na kule kwao zinakuwepo, masuala ya kilimo
kusafirisha mazao na namna ya utaalamu katika mambo mbalimbali ya
viwanda na biashara na vitu bora vinavyofaa kusafirishwa,” alisema.
Ujumbe huo utakuwepo nchini kwa siku tatu, pia watakutana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Wafanyabiashara
wa Oman wakiwa katika picha ya pamoja na balozi wa Tanzania nchini Oman
Mhe. Ali Ahmed Saleh (wa tano kushoto) na mwenyekiti wa baraza la
biashara Evarist Membe (wa tatu kushoto).
Balozi
wa Oman nchini, Mhe. Ali Ahmed Saleh (kulia) na mwenyekiti wa baraza la
biashara, Evarist Membe wakitoa maelekezo kwa wageni wao kabl;a ya
kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere.
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara nchini, Everist Membe akiwapokea wafanyabiashara kutoka Oma
-
0 comments:
Post a Comment