Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk
Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba.
Waziri Nchimbi alisema
upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo
tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya
mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo
uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini
Dar es Salaam leo.
Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na
waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na
uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu
Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha
waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa
kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi
Mjumbe wa Tume ya Katiba.
Katika msakao huo watuhumiwa tisa walikamatwa
wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu)
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.
Hata hivyo, Waziri
Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati
Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata
watuhumiwa wengine. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo