TAMWA,TGNP NA LRHS WAMTAKA PROFESSA JUMA KAPUYA AJIUZULU KUFUATIA KASHFA YA KUBAKA NA KUMUAMBUKIZA UKIMWI MWANAFUNZI

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Kituo cha Msaada wa Kisheria (LHRC), kimelaani viongozi wanaotumia madaraka yao, nafasi zao na nguvu zao kisiasa kuwadhalilisha watoto wa kike.

Mashirika hayo yanayotetea haki za wanawake na watoto, yamesema yamesikitishwa na habari zilizozoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu wasichana wawili wanaotafuta haki yao dhidi ya kiongozi wa kiserikali anayetuhumiwa kuwadhalilisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka

 "Mashirika hayo yanafahamu kuwa vitisho vilivyotolewa na kiongozi huyo vimewasababishia wasichana hao kuogopa kuishi nyumbani kwao kwa kuhofia maisha yao," ilisema sehamu ya taarifa ya pamoja ya mashirika hayo.


Iliongeza: “Tunashangazwa kuona hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika wakati wasichana hao wakitafuta msaada," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,  Valerie Msoka, katika taarifa hiyo.


Masharika hayo yametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuwalinda wasichana hao dhidi ya mtuhumiwa.
 
Aidha, ili kujenga imani na utawala bora, mashirika hayo yamemtaka mbunge huyo kujiuzulu mara moja.
 
Alisema Tamwa, TGNP na LHRC, yanawataka Watanzania kuungana na kupinga viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya. Watanzania wapige vita vitendo visivyo vya haki kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria