
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na familia ya Penny zimeeleza kuwa tukio hilo limezua sintofahamu kubwa kati ya pende mbili hali iliyosababisha wazee wa jadi kuingilia kati.
Aidha, imeelezwa kuwa masahibu yanayomkuta Diamond na Penny yanachangiwa na wawili hao kulila tunda lisilolika kutokana na damu zao kuwa moja...
Uchunguzi unaonesha kuwa mahusiano ya kimapenzi kati ya Penny na Diamond yaliibuka katika mazingira ya kutatanisha na tangu walipoingia katika mahusiano hayo furaha imekuwa ni ndogo kuliko majanga....
Chanzo hicho kilimweleza mwandishi wetu kuwa Penny ndo mtu wa kwanza kufikishiwa taarifa hizo mapema jumatano ya wiki hii hali iliyomfanya apoteze 'mudi' na kujikuta akitokwa na machozi...

Endapo undugu wa Penny na Diamond utathibitika kuwa ni wa damu,kuna hatari ya laana kuwashukia wapenzi hao kwani itamaanisha kuwa nje ya penzi lao wao ni kaka na dada wa damu...
Mpaka sasa kinachofahamika ni kwamba Penny ni mwenyeji wa Tanga wakati Diamond amekuwa akifahamika kama mwenyeji wa Kigoma kutokana na mama yake kuwa na asili ya Kimanyema.
Hata hivyo, kwa upande wa baba wa Diamond kumekuwa na taarifa nyingi tofauti ambazo hazijapatiwa uthibitisho.
Penny na Diamond hawakupokea simu zao walipotafutwa kutolea ufafanuzi skendo hizo.
-Gazeti la Kiu, toleo la leo