Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Sunday Demonte.
Aunt Ezekiel Grayson amefunguka kuwa alikwenda Dubai kwa mumewe Sunday Demonte kwa ajili ya kusaka mtoto kwani kwa sasa hatumii kinga kwa sababu anahitaji kuitwa mama.
Akiongea na Ijumaa Wikiend iliyopita, mara tu baada ya kutia maguu kwenye
ardhi ya Jakayaland mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo alilazimika
kurudi mapema kutokana na msiba wa rafiki yake kipenzi aliyemtaja kwa
jina moja la Sofia, Aunt alisema kuwa kwa sasa muda umefika wa kuzaa.
“Hata mume wangu anatamani sana mtoto, tumekaa na kukubaliana juu ya ishu hiyo hivyo muda wowote naweza kuwa mjamzito, japo siwezi kuweka wazi kama ni tayari au bado kuepuka wanga,” alisema Aunt Ezekiel.