Jeshi la Polisi nchini linapenda
kuutaarifu umma kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya
jinai (DCI) Robert Manumba amefikia umri wa kustaafu kisheria ambao ni
miaka sitini (60) katika utendani wake wa kazi.
Aidha, katika utumishi wake ndani ya Jeshi
la Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha
kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya
ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, (1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo
cha polisi Dar es salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya
Magomeni na Kinondoni na Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es
salaam (1987 – 1993),
Pia, amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa
wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi (
1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 –
1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya
kulevya makao makuu ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa msaidizi wa
mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 – 2006). Kuanzia
mwaka 2006 hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya
jinai nchini.
Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)
Said Mwema, amemshukuru na kumpongeza Manumba anayestaafu kwa
kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi
kwa weledi na uwaminifu mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi ndani ya
Jeshi la Polisi.
Pia, amemtaka kuendelea kuwa msaada kwa
Jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa namna yoyote ile unaoweza
kusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini kwasababu suala la usalama ni
taaluma kama zilivyo taaluma zingine, na taaluma hiyo wanayo watu
wachache.
Hata hivyo, wakati tataratibu wa uteuzi
wa mkurugenzi wa upulelezi ukiendelea, mkuu wa ufuatiliaji na tathimini
CID makao makuu, kamishina Isaya Mungulu, atakua akikaimu nafasi hiyo.