Jana wafanyabiashara wa nguo za ndani wa soko la Karume hawakuimaliza vizuri siku hiyo baada ya Shirikia la Viwango Tanzania[Tbs]kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini kuendesha operesheni ya Kataza kuuza nguo za ndani ambazo zishatumika(mitumba).
Afisa Habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi Roida aliongea
na waandishi wa habari mara baada ya kukamata kwa marobota hayo ya nguo
za ndani ambapo alisema wamekamata nguo hizo za ndani kwa sababu
walishazipiga marufuku kuuzwa hapa nchini kwa kukosekana kwa viwango
vinavyotakiwa lakini wafanyabiashara hao wamekua wakikaidi agizo hilo na
kuendelea kuuza.
0 comments:
Post a Comment