Kutoka kushoto: Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila,
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa TAMISEMI
Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), Ludovick Utouh wakiingia ukumbini leo mjini Bukoba.
Viongozi hao wakifungua kikao hicho cha kusomwa ripoti ya ukaguzi maalum ya CAG.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila akifungua kikao.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akimkaribisha mgeni rasmi leo
kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum " Exit Meeting" cha
CAG.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh akisoma ripoti ya ukaguzi maalum leo Bukoba.
Baadhi ya waliohudhuria kikao hicho.
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani (kulia) pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Bukoba katika kikao hicho. Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (kushoto) wakiteta
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bw. Fabian Massawe (kati) katika meza
kuu.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (katikati) akimsikiliza kwa makini Bw. Ludovick Utouh. Viongozi meza kuu wote walikuwa makini kusikiliza taarifa hiyo ya Ukaguzi. Taswira ya kikao hicho katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.Madiwani
wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Mstahiki Meya Anatory Amani ambaye
madiwani wa manispaa wanamtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
**
MEYA wa Manispaa ya Bukoba,
Anatory Amani amejiuzulu wakati Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Khamis
Kaputa na wakuu wa idara tatu ambao ni Mhandisi Nimzihilwa, Ofisa Ugavi
Baraka Marwa na Mweka Hazina Ulomi wakivuliwa uongozi baada ya ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh
iliyosomwa leo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera kutatua mgogoro
uliokuwepo katika manispaa hiyo.
0 comments:
Post a Comment