SOMO:- HIKI NDICHO KINACHOPELEKEA WANAWAKE WENGI KUTOPATA MIMBA...



TUNAPOSEMA tatizo la kutopata ujauzito ina maana mume na mke au watu walio katika uhusiano wa kutafuta ujauzito ndani ya mwaka mmoja lakini wameshindwa. Inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani kiwango cha chini ni mwaka mmoja..
Ni tatizo kubwa katika jamii kwani kila mmoja anataka afikie malengo ya kuwa na familia.  Mwanamke na mwanaume wote wanahusika katika tatizo hili, mara nyingi imeonekana ni tatizo la mwanamke.
CHANZO CHA TATIZO
Kutokushika ujauzito kwa muda mrefu ni ugumba au ‘infertility’. Mwanamke au mwanaume anaweza kuwa mgumba. Ugumba umegawanyika katika maeneo makuu mawili, kwanza ni ‘Primary Infertility’ ambapo mtu hana historia ya kuwa na mimba wala mwanaume hana historia ya kumpa mwanamke mimba.
Ugumba wa aina ya pili ni ‘Secondary infertility’ ambapo mwanamke anayo historia ya kuwahi kupata ujauzito, haijalishi kama alizaa au mimba ilitoka na mwanaume anayo historia ya kumpa mwanamke mimba pia haijalishi kama mtoto alizaliwa au mimba ilitoka.
TATIZO KWA MWANAUME
Tatizo la kutoweza kumpa mimba mwanamke linaweza kusababishwa na mwanaume kukosa nguvu za kiume hivyo kushindwa kufanya tendo la ndoa, hali hii ya kukosa nguvu inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali kwani yenyewe siyo ugonjwa.
 
Kwa hiyo kitu cha msingi siyo kuongeza nguvu bali ni kufanya uchunguzi kuona tatizo ni nini na kulipatia ufumbuzi.
Tatizo lingine kwa mwanaume ni kutotoa mbegu za kiume au kutoa mbegu zisizo na ubora. Hii ni baada ya kupimwa kipimo cha mbegu za kiume, mbegu zinaweza zisizalishwe au zikazalishwa pasipo na ubora unaostahili kurutubisha yai la mwanamke.
Matatizo mbalimbali yanaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume kama uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kali, maumivu ya korodani na utumiaji wa madawa ya kulevya kama mirungi na bangi.
 
Mazingira ya joto kali katika korodani pia huathiri uzalishaji. Tatizo hili na lile la upungufu wa nguvu za kiume tutakuja kuyaona kwa undani katika matoleo yajayo.
Kutokufahamu mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kipindi gani unaweza kumpa mimba pia ni changamoto katika tatizo hili kwa upande wa mwanaume.
UFUMBUZI KWA MWANAUME
Wanaume wengi huwa wagumu kufanya uchunguzi kuona kama wana tatizo au la, siyo kila unapoweza kufanya tendo la ndoa na kutoa manii kwamba huna tatizo, unaweza kutoa mbegu zisizo na ubora. 
Vilevile kuwa na historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na mtoto au watoto siyo kigezo cha kutokuwa na tatizo. Unaweza kuwa na historia hiyo nzuri lakini tatizo likaja kutokea baadaye.
 
Kwa hiyo unashauriwa na mwanaume ufanyiwe uchunguzi kuona kama una tatizo au hakuna. Uchunguzi kwa mwanaume ni kupimwa manii na vipimo vingine vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa. Tiba ipo endapo itathibitika tatizo ni uzalishaji au nguvu za kufanya tendo la ndoa. Kama tatizo ni ufahamu wa siku zipi za kushika mimba pia itaeleweshwa. Ni vema uwahi hospitali.
TATIZO KWA MWANAMKE
Kama ilivyo kwa mwanaume, mwanamke pia anahitaji uchunguzi wa kina, kwani tatizo linaweza kusababishwa na mambo mengi Matatizo yanaweza kuanzia ukeni yakapanda ndani au yakaanzia humohumo ndani.
-