Young Killer anasema pamoja na umri wake kumruhusu kuwa mrembo katika
maisha yake, bado hafikirii kuanzisha uhusiano na msichana kwa sasa.
“Umri wa kuwa na mpenzi nimeshafikia lakini sasa hivi nafanya mambo
yangu halafu baadaye naamini ntakuja kufanya hayo masuala, so sasa hivi
najipanga kwanza,” Killer aliiambia Bongo5. “Kusumbuliwa nasumbuliwa
sana tu sema kuna msemo mmoja ambao nakuambia wa Fid Q ‘Usiache
ulichotaka maishani ghafla tu na kufuata kile ambacho umetamani’.
Nimekuja kwaajili ya muziki, nilitegemea utanipa vitu vingi ila sio
mademu tu.”
Wakati huo Handsome Boy huyo asiye na matunzo, amesema video ya wimbo
wake ‘Mrs Supastaa’ iliyoongozwa na Adam Juma ni moto wa kuotea mbali.
“Ni video kali, naamini katika video zangu zote ile ndio
inaweza kuwa video yangu ya kwanza kufanya video kali. Naamini zingine
zitakuja ila ile kiukweli kali yaani,” alisema. “Nategemea mashabiki
wangu wataipokea vizuri kwasababu ni video nzuri, binafsi nimeridhika
nayo, sijawahi kufanya video kama ile.
0 comments:
Post a Comment