Barack na Michelle walikutana mwaka 1989 katika
mazingira ya kikazi, walifunga ndoa Oktoba 18, 1992, katika Kanisa la
Umoja wa Kristu la Trinity lililopo Chicago, Illinois.
Lakini vyanzo vingine vya taarifa zinadai kuwa ndoa haiko imara,
hasa baada ya tukio la Obama kupiga picha za pamoja bila aibu na Waziri
Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt (46) wakati wa mazishi ya
aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrka Kusini, Neslon Madiba Mandela.
Obama akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron, alikuwa akicheka na kumnong’oneza kitu waziri huyo mara kwa
mara kwa muda wote, huku Michelle akiwa pembeni yake amenuna. Mara
nyingi alikuwa akimshika shika mabega.
“Lakini kwa sasa Michelle anajiona kanyanyasika na
kuaibishwa mbele ya dunia kwani picha hizo zilirushwa duniani kote
kupitia televisheni, magazeti na mitandao mbalimbali. Alisikika
akimtapikia Obama huku akisema “Nimechoshwa.”
Pia tatizo limekuzwa na safari ya kikazi ya Obama
hivi karibuni kule Thailand ambayo ilimkutanisha na Waziri Mkuu mrembo
kuliko pengine wote duniani , Yingluck Shinawatra.
Tarifa zaidi zilieleza kwamba usalama wa taifa
nchini humo unafahamu kuhusu suala hilo, lakini umekuwa ukilichukulia
kama suala binafsi na Michelle alionekana kukasirishwa kupita kiasi
alipopata taarifa hizo.
“Baada ya tukio hilo Michelle aliamua kuwasiliana
na mwanasheria wake akitaka kujua namna ya kuomba talaka na alimwambia
Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye,” ilieleza sehemu ya taarifa
hiyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia,
ilielezwa kwamba Michelle ataendelea kuishi mjini Washington DC hadi
binti yao mdogo, Sasha (12) atakapomaliza elimu yake ya sekondari. Binti
yao mkubwa, Malia (15) tayari ameshaingia sekondari.
“Michelle (50) kwa sasa ataendelea kuishi kwenye
Ikulu ya Washington hadi Obama atakapomaliza muda wake wa urais ili tu
aweze kuonekana kama yupo, lakini aliweka wazi kabisa kwamba wataishi
maisha tofauti,” ilieleza ripoti hiyo ikimkariri mmoja wa vyanzo kutoka
Ikulu hiyo. Ripoti hiyo ilikariri chanzo hicho kikieleza; “Michelle kwa
sasa anaishi katika vyumba vya watumishi kwenye nyumba yao ya familia na
anajiandaa kuchukua vifaa vyake na kuvipeleka kwenye nyumba yao binafsi
ya Chicago”.
Taarifa nyingine ilieleza kwamba tayari mambo
baina ya wanandoa hao yameshakuwa magumu kiasi kwamba wamekuwa wakiishi
kwenye vyumba tofauti katika Ikulu ya Marekani.
Mgogoro wao
Barack na Michelle wamekuwa katika mgogoro kwa
miaka kadhaa na wanalazimika kuwepo pamoja kwa sababu tu ya watoto wao
na kulinda hadhi yake kisiasa. Lakini kwa sasa Michelle amekuwa mkali
kweli kweli. Anaona kama amepuuzwa na kudhalilishwa mbele ya dunia nzima
na amekuwa akipiga kelele akisema, “Nimevumilia vya kutosha”, taarifa
zaidi zilieleza.
Kwa sasa Michelle anaonekana kupigania kukamilisha
namna ya kupata talaka, lakini baadhi ya taarifa zinaeleza kwamba
anafanya makusudi kuuchelewesha ili aweze kuukamilisha baada tu ya Obama
kumalizia muda wake wa urais ambapo ataweza kupata Dola za Marekani 30
milioni kupitia mpango wa vitabu na zaidi ya dola 65 milioni kwa
kuonekana hadharani.
“Kwa sasa Barack anaonekana kama amemwaibisha Michelle mbele ya
dunia na kwa hili ni wazi kwamba atalilipa kwa gharama kubwa,” kilieleza
chanzo kutoka Ikulu ya Marekani.
“Ni jambio lililo wazi kwa sasa kwamba Michelle
ameshamwambia Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye, japokuwa kwa
sasa imekuwa ni suala gumu kwa kuwa anahitaji aendelee kuonekana wakiwa
pamoja kwa sababu muhimu, lakini wanapokuwa nyumbani wanaishi maisha
tofauti ya kutengana,” kilieleza chanzo hicho.
Iwapo taarifa hizo ni sahihi, hii inamaanisha
kwamba Michelle ameudhika kupindukia na hii si mara ya kwanza jambo hilo
kutokea miongoni mwao.
Tangu Obama alipochaguliwa kuwa rais, vitabu
viwili vimemtaja vikidai kwamba wenza hao walikaribia kutengana katika
kipindi cha miaka yao ya mwanzo ya ndoa na hata Michelle alifikia hatua
ya kutaka kuomba talaka akidai kwamba anaona maisha yake ya kisiasa
yanawanyima furaha na kuwa pamoja nyumbani.
Mwaka 2009 mwandishi wa siku nyingi wa Washington,
Richard Wolffe alisema kwamba ndoa hiyo ilikuwa sawa na iliyovunjika
miaka tisa kabla kutokana na harakati za kisiasa za Obama zilizokuwa
zikimsababisha asiwe karibu na familia kwa muda mrefu.
“Kulikuwa na mawasiliano kidogo sana na familia
yake na hata mapenzi yalipungua. Michelle alikasirishwa sana na hali
hiyo akilaumu kwamba mumewe anaonekana kuwa mbinafsi; ilimpa wakati
mgumu sana,” aliandika Wollfe.
Wakati huo Michelle alilazimika kutulia kwa kuwa
tayari alishakuwa mama, mbinti zao awili, Malia na Sasha kwa sasa wana
miaka 15 na 12. Mumewe ambaye walikutana kwa mara ya kwanza walipokuwa
wakifanya kazi kwenye shirika moja la sheria mjini Chicago mwaka 1989,
alikuwa ndiyo kwanza amechaguliwa kuwa Seneta wa Illinois na alikuwa
akijipanga pia kuwania nafasi kwenye baraza la Congress.
Mke wa Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas
Sarkozy, Carla Bruni alipoulizwa katika moja ya vitabu kuhusu uzoefu
wake wa maisha ndani ya Ikulu alijibu, ‘Acha kabisa! Usiulize ni kama
jehanamu. Sikuwahi kuyafurahia’ ambapo Michelle alisema hakuwahi
kuzungumza maneno ya aina hiyo.
Mwaka 2012 mmoja wa waandishi wa masuala ya siasa,
Edward Klein alieleza kwamba Obama alionekana mwenye mawazo kupita
kiasi, wakati ndoa yake ilipokuwa kwenye matatizo mwaka 2000 kiasi
kwamba rafiki zake walihofu kwamba anaweza kujiua.
Alieleza kwamba Michelle alikuwa mwenye hasira kwa
kuwa alimkataza Obama kuwania nafasi kwenye Congress, ushauri ambao
hakuufuata na hata hivyo alishindwa kwenye uchaguzi.
“Baada ya kushindwa alirejea kwa Michelle kwa
ajili ya kupata pumziko. Lakini Michelle hakuwa tayari kuonyesha huruma
yoyote,” aliandika Klein aliyedai kwamba marafiki wa Michelle
walimweleza kuwa tayari ameshafungua kesi akidai talaka.
-Mwananchi
0 comments:
Post a Comment