NAIBU
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Makongoro Mahanga
ameingia kwenye kashfa nzito ya kuvunja sheria za kazi nchini kwa
kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi yake Bunge kwa miaka kumi
bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi laki mbili tu (200,000)
kama mafao.
Naibu Waziri, Mahanga anakuwa kiongozi wa kwanza kuingia kwenye kashfa akiwa madarakani tena kwenye swala la ajira wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana na maswala ya ajira na haki za wafanyakazi nchini chanzo chetu kimeelezwa.
Kwa mujibu wa sheria kazi na mahusiano kazini, Naibu Waziri amekiuka kifungu cha 3 cha sheria ya Taasisi za kazi za mwaka 2004 na pia amekiuka sehemu ya tatu ya viwango vya ajira na sehemu ndogo A kwa kushidwa kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu cha 14 ibara ya kwanza kama sheria ya kazi na mahusiano kazini inavyotaka.

Katika kifungu hicho cha 14 ibara ya kwanza kinasema mkataba utakuwa wa kipindi cha muda usiotajwa, mkataba wa kazi maalumu na mkataba unatakiwa kuwa wa maandishi ambapo vyote Mhe Naibu Waziri hakufanya. Ibara ya 15 kifungu cha.-(1) kinasema kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 19, mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, wakati mfanyakazi anapoanza kazi, taarifa zifuatazo kwa maandishi, jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali alipoajiriwa; kazi zake; tarehe ya kuanza; muundo na muda wa mkataba; kituo cha kazi; masaa ya kazi; ujira na njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Bi. Itika Kasambala (31) anasema alianza kazi kwa Mbunge huyo wa Segerea na Naibu Waziri wa kazi Dkt. Mahanga, mwaka 2003 kama PS (Personal Secretary) kwa makubaliano ya kumpa mshahara wa shilingi 120,000 kwa mwezi lakini alianza kumlipa shilingi 50,000 tu.
“Aliniambia kwamba nianze kazi kwanza baadaye atanipa mkataba wa ajira na kunilipa mafao ya hifadhi ya jamii na matibabu lakini baada ya miaka kumi ananitumia sms akiwa Dodoma kwamba kazi basi sikuhitaji tena,” Kasambala alisema.
Amesema kwamba Mbunge huyo alimtumia sms akiwa kwenye vikao vya bunge mjini dodoma mwaka jana mwezi wa sita akimjulisha kwamba ajira yake imeshafika kikomo kwa sababu hana uwezo tena wa kumlipa mshahara na mahitaji mengine ya kiofisi.
0 comments:
Post a Comment