Mwigulu Nchemba awajibu watanzania wanaomponda baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha.., Soma Hapa Alichokisema


Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye juzi alikuwa miongozi mwa manaibu waziri walioapishwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nyadhifa zao amewaambia watu wanaoponda uteuzi wake kuwa hana haja ya kubishana nao kwani hawamjui. 

Katika maelezo yake, Mwigulu alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini. 

"Watu wasionifahamu wanadai mimi sina viwango vya kufanya kazi hii; naomba wafahamu kuwa mimi ni msomi mwenye shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko katika masomo ya kupata shahada ya uzamivu." Alisema  Mwigulu  na  kuongeza:
 
 “Kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania kama mchumi. Ninakwenda Wizara ya Fedha kusimamia mambo manne ambayo ni uadilifu, ushirikiano, jitihada na huduma madhubuti ambazo zitatolewa kwa wakati mwafaka."

1 comments:

Anonymous said...

Congratulation mwigulu, unaweza kabisa,