Warembo wanaotoa huduma wakiwa wameficha sura zao baada ya kunaswa na OFM.
Hebu sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini
kumbe ngono imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa
uchafu wa aina yake nyuma ya pazia.Saluni hiyo maarufu kuliko Miji ya Sodoma na Gomora, ipo maeneo ya Sinza ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikijihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yaliyotukuka.
TAARIFA MEZANI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, ikiwa imetulia ndani ya mjengo wa makao yake makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar, Mkuu wa kikosi maalumu cha Mtambo wa Kurekebisha Tabia (MKT) ambacho ni kitengo ndani ya OFM, alipokea simu kutoka kwa msamaria mwema akitoa ‘tipu’ juu ya ishu hiyo.
Mhudumu baada ya kumpatia dozi mteja.
Mtoa taarifa huyo alieleza malalamiko yake juu ya kero wanayoipata
raia waishio jirani na saluni hiyo kufuatia huduma chafu za kuchukiza
ambazo hufurahiwa na shetani na malaika wake tu.Msamaria Mwema: Halooo.... halooo... jamani halooooo, hapo ni Makao Makuu ya OFM?
OFM: Ndiyo mama, tukusaidie nini?
Msamaria Mwema: Mna habari jamani?
OFM: Zimejaa tele, ila hata ya kwako inaweza kuwa bora kuliko tulizonazo.
Msamaria Mwema: Hapa Sinza Kwaremi (Dar) kuna saluni moja inaendesha vitendo vichafu vya ngono na hakuna sheria yoyote inayochukuliwa dhidi ya wahusika.
...Huyu alinaswa akikimbia baada ya OFM kutia maguu eneo la tukio.
OFM: Saluni ya ngono? Kivipi mama? Hebu fafanua tafadhali!Msamaria Mwema: (kwa sauti ya juu mno) ninyi njooni mtajua kila kitu hukuhuku lakini inaendesha mambo ya ajabu (simu ikakatika).
OFM MZIGONI
Bila kupoteza sekunde, mkuu huyo wa MKT, aliwapanga ‘makamanda’ maalumu na kuwapa maelekezo muhimu ya jinsi ya kujua ukweli juu ya uovu uliodaiwa kutendwa kwenye saluni hiyo.
UCHUNGUZI
OFM iliwatuma vijana wake ‘watanashati’ hadi eneo lililotajwa ili wachunguze kama kweli kuna saluni yenye jina lililotajwa na mtoa habari wetu.
Baada ya maelekezo hayo, vijana hao wakiongozwa na roho safi ya kunyoosha maadili katika jamii, walifika hadi Sinza na kukuta saluni yenye jina hilo ambapo walianza kufanya upelelezi wa hali ya juu mno huku wakiwa makini kuliko hata neno lenyewe.
UTHIBITISHO
Baada ya kutinga eneo hilo, OFM iliendesha upelelezi maalumu kwa kuwauliza baadhi ya wakazi na watu wanaofanyia shughuli zao za kujiingizia riziki na kupata ukweli halisi juu ya ufuska ufanywao ndani ya saluni hiyo.
Katika uchunguzi huo, OFM ilipata uthibitisho kuwa kweli ibilisi yuko katika hesabu zake za mwaka kwa kufanya uchafu wa kufuru.
Ilielezwa kwamba, watumishi wa saluni hiyo ambao ni warembo, hujifanya wanatoa huduma ya kuchua mwili (body massage) kwa Sh. 25,000/= kwa vyumba na huduma za kawaida, lakini kwa vyumba vyenye choo na bafu kwa ndani (self contained) ni Sh. 35,000/=.
HUDUMA
Katika upelelezi huo, ilibainika kuwa mteja akilipia gharama ya vyumba vya self contained, ana uhuru wa kuchagua kama atapenda kufanyiwa huduma ya uchuaji kwa mikono tu au kwa matiti na wakati mwingine mwili mzima huku mtoa huduma hiyo akiwa amevua nguo zote!
Ikazidi kuelezwa kuwa, endapo mhudumiwaji atataka huduma hiyo ya mchuaji kuvua nguo zote, atafanyiwa hivyo lakini kama atazidiwa na kuhitaji huduma ya ngono, atatakiwa kuongeza Sh. 50,000/= kwa msichana huyo wa huduma na kufanya gharama kuwa zaidi ya Sh. 80,000/=.
“Wamekuwa wakifanya vitendo viovu sana, yaani ngono njenje, jamani hii siyo saluni, bali ni danguro la ngono fuatilieni mtangundua juu ya ukweli huu,” alisema mmoja wa raia katika upelelezi wa OFM.
OFM NDANI YA NYUMBA
Ili kujiridhisha na maelezo hayo, timu ya OFM ilituma vijana wake tofauti kwa muda wa siku tatu mfululizo na kubaini kuwa yote yaliyosemwa na kutajwa kwa kirefu yanatendeka ndani ya saluni hiyo!
‘Askari’ wa kwanza wa OFM aliingia ndani ya saluni hiyo (jina linavunda kwenye droo za meza yetu) na kuwakuta wahudumu wamejaa tele na alipowauliza juu ya huduma ya masaji na ngono, walijibu kwa sauti ya furaha na bashasha kubwa bila kujua kuwa kijana wetu alikuwa na vifaa maalumu vya kunasia sauti.
“Ni wewe tu jamani, kwani wewe ni mgeni maeneo haya? Mbona utaratibu unaeleweka, lakini maelezo ni hayo kwa hiyo karibu sana,” alisema mmoja wa warembo hao huku akilegeza macho mithili ya mgonjwa wa degedege.
Siku mbili zilizofuata, askari wa OFM waliendelea kupata stori na maelezo ya aina hiyohiyo.
MTEGO!
Siku ya tukio, (mwanzoni mwa wiki hii) OFM iliweka mtego kwa kumpeleka kijana wake ili ajifanye anahitaji huduma hiyo ya kufanyiwa masaji mwili mzima na baadaye ajifanye amezidiwa na kuhitaji huduma ya ngono.
Katika mtego huo, OFM ilitoa taarifa polisi ambapo ‘vijana wa IGP Ernest Mangu’ hawakulaza damu, wakatoa ushirikino wa kutosha kwa OFM.
MTEGO WAFYATUKA
Kama kawaida, OFM huwa haishindwi linapokuja suala la oparesheni maalumu kama hiyo, fuatilia sana. Mtego wake ulifyatuka ambapo mmoja wa vijana wake alijifanya kuhudumiwa (angalia picha ya mwanzo).
Baada ya kuweka mazingira sawa, OFM na polisi wa kike na kiume walivamia na kufanikiwa kufuma laivu matukio mengi ya ufuska mkubwa (ukitaka kuona zaidi, unakaribishwa Bamaga ofisini kwetu).
WAUME ZA WATU!
Baada ya zoezi hilo kukamilika, baadhi ya mashuhuda (hasa akina mama) walisikika wakishukuru kufumuliwa kwa saluni hiyo kwa kuwa ndoa zao zilikuwa zimeanza kuota magugu kwani wateja wengi wa saluni hiyo ni waume za watu na vigogo serikalini!
“Jamani tunashukuru sana, waume zetu walikuwa wanakimbilia hapo, ugomvi kidogo tu, mwanaume anakwenda hapo na akirudi nyumbani hana habari kabisa na mkewe, safi sana OFM na polisi kwa jumla,” alisikika mama Joyce akishangilia kufumuliwa kwa saluni hiyo.
SOO POLISI
Baada ya ‘sheshe’ hilo, warembo sita walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa upelelezi maalumu.
MMILIKI
Katika upelezi wa awali, watumishi hao walimtaja mmiliki wa saluni hiyo kwa jina moja la Chifu huku wakishindwa kuweka wazi na kufafanua kwa undani zaidi.
KAMANDA WAMBURA UPO?
Gazeti hili lilifanya jitihada za hali ya juu kumpata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura ili azungumzie juu ya sakata hilo, lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa.