Bibi kizee mmoja mwenye umri wa mika 65 ameuawa
kikatili kwa kukatwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na
kusababisha kifo chake katika eneo la Kigogo Mburahati national housing
jijini Dar es Salaam.
Kutokana
na tukio hilo la kikatili aliofanyiwa bibi huyo kizee aliyefahamika kwa
jina na Bi Asia Mohamed maarufu kwa jina la bibi Chadego, Paparazi wetu
alifika nyumbani kwa bibi huyo mwenye umri wa miaka 65 na kuzungumza na
mjumbe wa eneo hilo bi Hidaya Salum na kusema bibi huyo ameuawa
kikatili akiwa nyumbani kwake huku mtoto wa marehemu naye akieleza
kusikitishwa na kifo cha mama yake.
Baadhi
ya wasamaria wema ambao hawakutaka kutaja majina yao kwa usalama
wao,wamesema bibi huyo alikuwa akihusishwa na mambo ya ushirikina na
baadhi ya familia yake baada ya vifo vya wajukuu wake watatu ambao
walifariki kwa nyakati tofauti kipindi cha nyuma ambao licha ya kudaiwa
wajukuu hao kufariki kwa mambo ya kishirikina lakini ukweli ni kwamba
bibi huyo hakuwa mchawi wala hakuhusika na vifo hivyo huku ikidaiwa
kwamba bibi huyo hakuuawa na mjukuu wake kama inavyodaiwa ila kuna
mchezo uliochezwa na watu fulani ili kumuua na kisha kugeuza kuwa ni
mjukuu wake mwenye tatizo la akili.
Kamishna
msaidizi wa polisi kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni ACP Camilius
Wambura,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba licha ya mjukuu
wa bibi huyo kushikiliwa na jeshi la polisi kwa madai ya upotevu wa
godoro lakini upepelezi wa uhakika bado unaendelea kuhusu tukio hilo
hivyo wananchi wameombwa kutoa ushirikiano ambapo pia mganga mkuu wa
hospitali ya mwananyamala dakta Sophinias ngonyani amekiri mwili wa
marehemu kuhifadhiwa katika hospitali hiyo.