Maandamano ya wapenzi wa jinsia moja India
Mahakama ya juu kabisa nchini India, imetaka
kuendelea kwa sheria inayowatia hatiani wapenzi wa jinsia moja, uamuzi
ambao unaonekana kuwa pigo kwa haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya
jinsia moja.
Uamuzi wa mahakama hiyo unabadilisha uamuzi wa
Mahakama Kuu ya Delhi uliofanyika mwaka 2009, ambapo mahakama hiyo
iliona si uvunjaji sheria kwa watu wanaoshiriki vitendo vya wapenzi wa
jinsia moja.
Mahakama hiyo ya juu imesema ni jukumu la bunge kutunga sheria kuhusu suala hilo.
Kwa mujibu wa kifungu cha 377, sheria ya
kikoloni iliyodumu nchini India kwa miaka 153, uhusiano wa kimapenzi kwa
wattu wa jinsia moja ni kosa lisilo la kawaida na adhabu yake ni
kifungo cha miaka kumi jela.
Vyama kadha vya kisiasa, makundi ya kijamii na
kidini nchini India, katika mkesha wa kutolewa hukumu juu ya suala la
wapenzi wa jinsia moja, mwaka 2009, waliitaka mahakama hiyo kuendelea
na sheria inayopiga marufuku vitendo vinavyowashirikisha wapenzi wa
jinsia moja.
Vyombo vya habari vinasema japokuwa sheria hiyo
ndra ilitumika, kama iliweza kutumika kuwashitaki watu wanaojihusisha na
mapenzi ya jinsia, mara kwa mara sheria hiyo ilitumiwa na polisi
kuwanyanyasa wapenzi wa jinsia moja. Pia kwa India iliyojikita katika
utamaduni na mila, uhusiano wa jinsia moja ni mwiko na watu wengi
wanaona uhusiano wa jinsia moja si halali.
'Ni siku ya giza'"Ni juu ya bunge kutunga sheria
kuhusu suala hili," Jaji GS Singhvi, mkuu wa jopo la majaji wawili wa
Mahakama ya juu kabisa nchini India, amesema katika kutoa hukumu ya
Jumatano, ambayo imetolewa