HIVI NDIVYO LOWASSA ALIVYONUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA NDEGE YA PRECISION AIR BAADA YA KUPASUKA MATAIRI YOTE MANNE HUKO ARUSHA!

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa. ABIRIA kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha mchana mchana huu.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua. Matairi yote manne ya nyuma yamepasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Lowassa ni miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuwania urais 2015 na amekuwa na nguvu kubwa katika harakati hizo.
SHUHUDA ANASEMAJE? 
"Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.
Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!
Rubani wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa njia hiyo.
Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa"