Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo wafanyabiashara wamesusia Maadhimisho ya Siku ya Mlipa Kodi
yaliyofanyika mkoani Lindi wakipinga kushinikizwa kutumia
mashine za risiti za TRA (EFDs).
Akiongea na Mwandishi,
mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Kilimo na Viwanda Chris Miwa
amesema kuwa wamefikia uamuzi huo kwa kuwa hawana imani na Mamlaka ya
Mapato Tanzania.
Vilevile, wawakilishi wa wafanyabiashara
wadogo wadogo waliofunga maduka juzi kugomea mashine hizo wamesema
wanahofia kufilisika kama TRA itaendelea kuwalazimisha wanunue EFDs,
kwani mitaji yao ni midogo hivyo hawatamudu gharama hizo.
Mgomo
huo baridi ulipeleka waandaaji wa maadhimisho hayo kubaki wameduwaa
mchana wa leo pale walipojikuta wakiwa wenyewe ukumbini hoteli ya Double M,
huku mamia ya wafanyabiashara waliowaalika wakishindwa kutokeakatika mkutano huo.