Mtangazaji/Mwandishi wa siku nyingi
ndani na nje ya mipaka ya Tanzania Tido Mhando ameyatoa ya moyoni kuhusu
Mbunge mmoja wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambae
hajapendezwa na mwenendo wake.
Ishu ilianzia kwenye headline ya
kuwasema Waandishi wa habari ambapo namkariri Tido akisema ‘kuna
wengine miongoni mwetu ambao wanachukua nafasi hizi kujaribu kutafuta
njia za kujipenyeza ili waweze kujenga majina yao na kuharibu ukweli wa
fani yetu, tunawafahamu baadhi yao.. kuna wengine wamefikia hatua hadi
kuingia mjengoni na huko wanatamka maneno ambayo kwakweli huwezi kuamini
kama walikua Waandishi wa habari’
‘Mfano kuna mwenzetu mmoja yuko pale
(bungeni) na bahati mbaya kauli zake ni kutusema Waandishi wa habari
kitu ambacho sidhani kama ni kweli, kwanza mwenyewe sielewi kama ni
kweli kwamba aliwahi kuwa kwenye kitengo cha Propaganda BBC, nimekua BBC
kwa miaka 20 nilikua kiongozi wake, hata siku moja sikuwahi kukiona
kitengo hicho cha Propaganda…. wala si hivyo, sidhani kama yeye mwenyewe
alishaeleza ukweli kwamba alikua vipi pale BBC, ni wazi aeleze kwamba
kweli aliwahi kuajiriwa na BBC au alichukuliwa tu kwenda kusoma habari,
sasa kama kusoma habari ndio kujiita mwandishi wa habari basi inabidi
aeleze’ – Tido
Kwa kumalizia, Tido amesema ‘na labda
mwishoni aeleze ni kwanini hatimae aliamua kuondoka BBC, sasa kiasi hiki
cha Makanjanja ambao tutawaruhusu waingie na hatimae kuwapa hali ambayo
kwakweli inakua na maana potofu kwetu, hali hii inatuharibia na kamwe
tusiwakubali watu hawa waingie wawe miongoni mwetu, watu hawa
wameidhalilisha sana sekta ya habari na ni wajibu wetu kuhakikisha
waandishi wote wana uwezo wa kweli kufanya kazi hii na pia tukubali
kwamba endapo chombo cha habari au mwandishi amekosea, kuna vyombo
ambavyo vimewekwa kufatilia makosa yetu’