MWANAMKE AJITIA KITANZI KWA KUTUMIA MTANDIO WAKE..!!

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema

MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Maria Evansi (42) mkazi wa Kijiji cha Kaswira, Nanjara Kibaoni, Tarafa ya Tarakea wilayani Rombo amekutwa akiwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mtandio chumbani kwake.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Rombo, OCD, Ralph Meela, amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa nne asubuhi. Shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mtoto wa marehemu, Thea Evans aliuambia mtandao huu kuwa asubuhi aliondoka nyumbani akamwacha mama yake (marehemu) akiwa mzima lakini ghafla alishangaa aliporudi alimkuta akiwa ananing’inia juu ya paa ya nyumba yake akiwa tayari amekwisha fariki.

Hata hivyo, chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika kwani marehemu hakuacha ujumbe wowote, lakini inasemekana kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili kwa muda mrefu. Aidha habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu alishawahi kujaribi kujinyonga kwa zaidi ya mara nne kwa vipindi tofauti.