Habari,
Mimi
nimeoa na ndoa yangu ina miaka 7 sasa na tuna watoto wa 2. Nilimuoa
mwanamke aliyekuwa kamaliza degree ambaye alikuwa home tu at the time
anatafuta ajira.
Toka nimuoe hajawahi kufanya kazi yoyote ile yaani
Goalkeeper mpaka leo na kutafuta kazi alisha acha. Mpaka leo hii mke
wangu hajabadilika. Namlipa mshahara mwisho wa mwezi ambao ni sawa na
kama 10k per day yaani (300k).
Kila ninapojaribu kumtafutia kazi
anafanya kidogo tu anaacha. Huwezi amini hata umlazimishe vipi
ajishughulishe mzito ile mbaya. Mi ni mfanyabiashara nimemuanzishia vimiradi through the years vyote kala mtaji.
Kuna kipindi
alijaribu kusoma masters ya bussiness administration nkamlipia ada,
nunua vitabu vyote alafu yeye akaamua kuacha baada ya mwezi tu Eti
kuamka alfajiri hawezi. Nkaja nkamuomba basi asome chuo ambacho atakuwa
anaingia mchana nacho alishindwa.
Tatizo
rafiki yake mkubwa ni mama yangu mzazi hivo kuna kipindi nlikata
mshahara wake ili kumlazimisha afanye kazi akakimbilia kulia manyanyaso
nikalazimishwa hela yake isiguswe na wazazi wangu. Nkienda kazini
namuacha nyumbani na home kwenyewe hafanyi chochote anaita tu housegirl.
Yaani yupo yupo tu siku hadi siku. Nifanyaje ili hata nikianguka leo au
kesho awe ni mama atakayeweza kusomesha watoto.
Alafu
matumizi yake ya hela mabaya yaani hela yake mwenyewe ukimpa mwanzo wa
mwezi kwenye tarehe 1 hiv basi ikifika tarehe 8 ujue alikuwa anaumwa.
Ila ni hela yake na hainunui hata nguo ya mtoto hivyo hainihusu.
Nifanyaje ajishughulishe?