HIKI NDICHO ALICHOKISEMA ZITTO KABWE KUHUSI KIFO CHA DK. SENGONDO MVUNGI...

Tume ya mabadiliko ya katiba imepatwa na janga kubwa kufwatia kifo cha Dr Sengondo Mvungi ambaye alikuwa ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba. Dk Sengondo Mvungi amefariki dunia jana nchini Afrika Kusini ambako alipelekwa kupatiwa matibabu katika hospitali ya Milpark.

 
Kupitia ukurasa wa facebook wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe alisema “Mola anatuambia nini kwa mtihani wa kifo cha dkt. Mvungi? Allah hawezi kutuchukulia Mwalimu wetu kwa namna hii bila sababu. Bwana hawezi kumchukua baba yetu kwa njia hii bila somo kwetu. Huu ni mtihani mkubwa. 

Kama Mwalimu aliyebobea, mjumbe wa tume ya katiba anaweza kuvamiwa na kupigwa hatimaye kufariki, vipi kuhusu mwananchi wa Kalinzi au Kidahwe?

Ni mtihani.