Showing posts with label JACKLINE WOLPER. Show all posts
Showing posts with label JACKLINE WOLPER. Show all posts

HIVI NDIVYO AUNT EZEKIEL, WOLPER, SNURA WALIVYOFUNGA MTAA KWA MAUNO..!!

Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary.
 
Snura Mushi.
Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.
Aunt Ezekiel.
“Yaani wewe ulikosa mambo,  Snura alitoa shoo na mapacha wake utadhani alikuwa amelipwa, yaani walinogesha ngoma ya kumuaga mdogo wake Vanitha ambaye anakwenda kufunga ndoa Dodoma,” alisema sosi aliyekuwa akimsimulia mwandishi wetu.
Jack Wolper.
Aidha, wageni waliokuwa wamealikwa eneo hilo hawakudhani kama Wolper na Aunt wangeweza kujituma vile kama walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa sababu ustaa wote waliuweka pembeni na kujiachia kwa raha zao.
Continue Reading...

JACKLINE WOLPER ANENA BAADA YA KUBADILISHA DINI KWA MARA YA 2, SOMA HAPA ALICHOKISEMA..


Muigizaji wa filamu za  kibongo  maarufu  kwa  jina  Jackline Wolper  ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. 

Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.

“Mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.

Kitu Muhimu nikuwajuza nakuwaelewesha mashabiki wangu staki maswali nawapenda wote…”

Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.

Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?

Continue Reading...